Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akifungua mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo makamishna/wajumbe wapya na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC). Mafunzo hayo yanahusisha wajumbe wapya wa Tume za Uchaguzi na maafisa kutoka nchi tisa wanachama wa Jukwaa la ECF-SADC ambazo ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botswana, Namibia, Zimbabwe, Lethoto, Malawi na Tanzania na yameanza leo Novemba 22 hadi 25 ,2022 jijini Dar es Salaam.
Mwekiti wa Jukwaa la ECF-SADC ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Namibia, Elsie Nghikembua akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo wajumbe wapya wa Tume za Uchaguzi na maafisa kutoka nchi tisa wanachama wa Jukwaa la ECF-SADC ambazo ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botswana, Namibia, Zimbabwe, Lethoto, Malawi na Tanzania wanashiriki mafunzo hayo ya siku nne.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mabruki Makame akizungumza nebo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo Novemba 22,2022.
Mgeni rasmi wa ufunguzi wa mafunzo kwaajili ya Makamishna /Wajumbe na Maofisa waandamizi kutoka Tume za Taifa za kutoka nchi wanachama wa ECF-SADC, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele (katikati) wakiwa katika ufunguzi huo leo jijini Dar es Salaamz. Kushoto ni Mwekiti wa Jukwaa la ECF-SADC ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Namibia, Elsie Nghikembua na Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera Charles.
Makamishna/Wajumbe na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC) wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.
Olufunto Akinduro akiendesha mjadala wakati wa mafunzo hayo.
Harris Patani akiongoza mijadala wakati wa mafunzo hayo.
Makamishna/Wajumbe na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC) wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo.
Picha za pamoja za viongozi na washiriki
**********
Jukwaa la Tume za Uchaguzi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (ECF – SADC) kwa kushirikiana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Taasisi ya International IDEA wameandaa mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo Makamishna wapya na maafisa waandamizi wa Tume ambazo ni wanachama wake.
Mafunzo hayo yaliyoanza leo Novemba 22,2022 jijini Dar es Salaam yanataraji kufikia tamati Novemba 25, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema nchi 9 wanachama wa Jukwaa la ECF-SADC ambao ni Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botwana, Namibia, Zimbabwe, Lesotho, Malawi na Tanzania wanashiriki mafunzo hayo.
Aidha Jaji Mwambegele amesema baadhi ya nchi ikiwemo Afrika kusini zitashiriki katika mafunzo haya kwa njia ya mtandao (Virtually).
Amesema wajumbe na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatawasaidia katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yao.
“Washiriki watajifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ambayo uchaguzi umekuwa ukifanyika katika nchi zao na kuona changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza na namna ya kuzitatua,”alisema Jaji Mwambegele.
Aidha Jaji Rufaa Mwambegele amezitaja mada zitakazowasilishwa katika mafunzo hayo kua ni pamoja na demokrasia, uchaguzi na menejimenti ya uchaguzi; Vigezo vya kimataifa vya upimaji wa uchaguzi na wajibu wa kuendesha chaguzi za kidemokrasia; Usimamizi wa uchaguzi: Tafsiri, mifano, majukumu na na nguvu ya kisheria.
Mada nyingine amezitaja kuwa ni pamoja na Mifumo ya uchaguzi, Mzunguko wa uchaguzi, kalenda ya uchaguzi na mipango ya uchaguzi, Matumizi ya TEHAMA katika chaguzi, Masuala yanayojitokeza katika usuluhishi wa migogoro ya uchaguzi na utoaji haki za katika uchaguzi na Uandikishaji wa wapiga kura.
Pia zipo mada za siku ya uchaguzi (kupiga kura) na menejimenti ya matokeo, Changamoto kwa Tume za Uchaguzi, Uongozi wa Tume za Uchaguzi, utendaji kazi na uendelevu wake, Ushawishi kwa Wadau wa uchaguzi, changamoto na uhusiano na Tume; Kuendesha Uchaguzi Jumuishi kwa kuzingatia jinsia, vijana na watu wenye ulemavu.
Jaji Rufaa Mwambegele amezitaja mada zingine kuwa ni pamona na Menejimenti ya mashinikizo ya kisiasa;, Kugharamia uchaguzi na Tume za uchaguzi ; Ushirikiano kati ya Tume za uchaguzi na vyombo vya habari na mawasiliano ya nje ya taasisi pamoja na masuala yanayojitokeza katika sekta ya mawasiliano ya
Mada za Kukabiliana na majanga na kujenga uwezo wa namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza na Usalama wakati wa uchaguzi, vurugu na namna ya kutatua changamoto pia zitatolewa.
“Baada ya kupatiwa mafunzo ni matarajio kuwa watendaji hawa watakwenda kuhakikisha kuwa chaguzi zinakuwa huru, za haki na zenye kuaminika. Hii itasaidia katika kukuza demokrasia itakayochochea amani, usalama na ustawi wa wananchi na Taifa,”alisema Jaji Rufaa Mwambegele.
Toa Maoni Yako:
0 comments: