Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luanda wilaya ya Kalambo leo kuhusu ukamilishaji wa miundombinu ya shule shikizi ili wanafunzi wasome kwenye mazingira bora ambapo ameitaka halmashauri hiyo kupeleka mwalimu na kuweka madawati. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Tano Mwera.
Sehemu ya majengo ya hospitali ya wilaya ya Kalambo ambayo pamoja na mengine yamegharimu shilingi Bilioni 3 tangu yalipoanza kujenga 2018 lakini hayajakamilika hivyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga (hayupo pichani) ameagiza viongozi wa wilaya hiyo wajitathmini juu ya utendaji waoMkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akisalimiana na mama mwenye mtoto mdogo leo wakati alipokagua ujenzi wa kituo cha afya Kanyezi wilaya ya Kalambo ambapo amewahakikishia kukamilika kituo hicho ndani ya siku 14 zijazo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga (katikati) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwera (kushoto) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Ibrahim Isaack leo alipotembelea kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya Kalambo na kutoridhishwa na mradi huo kutokamilika kwa wakati.

(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: