Mhifadhi mkuu wa hamba la miti la Sao Hill Lucas Sabida akiongea na waandishi wa habari juu ya utalii huo mpya wa mchezo wa mbio za magari katika msitu wa shamba hilo.
Mhifadhi mkuu wa hamba la miti la Sao Hill Lucas Sabida akiongea na waandishi wa habari juu ya utalii huo mpya wa mchezo wa mbio za magari katika msitu wa shamba hilo.
Mhifadhi mkuu wa hamba la miti la Sao Hill Lucas Sabida akiongea na waandishi wa habari juu ya utalii huo mpya wa mchezo wa mbio za magari katika msitu wa shamba hilo.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill mkoani Iringa wameanzisha utalii wa michezo ya magari katika shamba hill kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kutangaza utalii wa ndani kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyofanya kwenye filamu ya Royal Tour.
Akizungumza wakati wa kutangaza kwa mashindano ya magari katika shamba la miti la Sao Hill, Mhifadhi mkuu wa shamba hilo Lucas Sabida alisema kuwa wamejipanga kuanzisha utalii katika shamba hilo ambao utaongeza kipato kwa wananchi na shamba hilo.
Sabida amesema kuwa kwa sasa wameanzisha utalii wa mchezo wa magari ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 11/09/2022 katika shamba la miti la Sao Hill na wananchi wote wanakaribishwa kwenda kutazama mchezo huo.
Alisema kuwa wao kama Shamba mbali na kujihusisha na shughuli za mazao ya isitu lakini pia wanafanya shughuli za utalii wa michezo ambapo kwa mara ya kwanza wameanza na utalii wa Mbio za Magari ambayo yatafanyika September 11 Mwaka huu.
"Leo tumekutana kwa lengo la kujiridhisha na kuangalia maandalizi hatua ambayo tumefikia hadi sasa sanjari na kukagua njia zote ambazo zitatumika kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu ni zoezi ambalo halijawahi kufanyika katika historia ya shamba letu hivyo ni kitu kipya." Amesema Sabida
Sabida alisema kuwa katika Shamba hilo kuna barabara ambazo wamekuwa wakidhihifadhi ambazo zinaurefu wa kilometer 1500 hivyo ni fursa ya kipekee ya kutumiwa kwa utalii wa michezo ambayo ni mchezo mpya
kwa upande wake Mwenyekiti wa Mbio za Magari kwa Mkoa wa Iringa Amjad Khan amesema kuwa Sao hill na wao kwa pamoja wameshirikiana kuandaa Mashindano hayo madogo ya magari ambayo huitwa sprint kwa ajili ya kujifunza kuhusu Shamba hilo
" Hadi sasa tumejipanga vizuri na maandalizi yamefikia asilimia 99 kwa sababu tulijipanga vizuri ili kuhakikisha Mashindano hayo yanafanikiwa kwa sababu tulianza kujiandaa mwezi mmoja na nusu kabla ya siku hii ambayo tunazungumza na waandishi ikiwa kila kitu kimekamilika." Amesema Khan
Amesema kuwa Mashindano hayo ni fursa nzuri kwao ya kushirikiana na Serikali kuweza kutangaza msitu huo ili watu waweze kuelewa zaidi pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kutangaza masuala ya utili ikiwa utalii wa michezo.
"Malengo ya Mashindano hayo ya magari ni kutangaza msitu wa sao hill hivyo Iringa motorsports Club tumepata fursa hii hivyo .. Sisi kama club tumefurahi sana... Kwa bahati ambayo tunaipata na tumeipokea kwa mikono miwili na tunajisikia furaha sana." Amesema Khan
Naye Mchezeshaji wa mchezo huo wa magari John Makeo alisema asilimia kubwa wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa shamba kwakuwa ni mara ya kwanza kushiriki michezo huo katika Shamba hilo.
"Watu wengi wa Mafinga walikuwa wanakuja Iringa kwa ajili ya kuangalia Mashindano hayo lakini September 11 yatafanyika katika Msitu wa shamba la Sao hill ambapo wataweza kujionea fursa zilizopo na kuzitangaza ikiwemo utalii wa nyuki pamoja na gundi zipo katika msitu hii" Amesema Makeo
Hata hivyo katika Mashindano hayo jumla ya madereva zaidi ya 20 wanatarajiwa kushiriki katika mchezo huo ambapo hadi sasa wanajumla ya washiri 14 ambao wamekubali kushiri kwenye mchezo huo watazungumza mizunguko minne ambayo Sawa na kilometer 6.
Sabida amesema kuwa SAO HILL MISITU AUTO CROSS ni zao jipya la Utalii ndani ya Shamba la Miti SaoHill Mafinga TFS wanasema utalii wa aina hii ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya Shamba la Miti SaoHill
Toa Maoni Yako:
0 comments: