Kamishna wa uhifadhi Wakala wa huduma za misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo akibadilishana mawazo na mdau wa TFS, (picha na Jane Edward.)
Naibu waziri Akiteta jambo na viongozi wenzake katika eneo la maonyesho ya Utalii EAC.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suhulu Hassan kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi,Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeanza kutoa ofa kwa wananchi wa jumuiya ya Afrika mashariki kutembelea maeneo ya Ikolojia na kujionea fursa zilizopo.

Kauli hiyo inatokana na kuwepo kwa maonyesho ya kwanza ya utalii yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika mashariki kwa kushirikiana na jamhuri ya muungano wa Tanzania, yaliyofanyika Makao makuu ya jumuiya hiyo Mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa Habari Kamishna wa Uhifadhi Profesa Dos Santos Silayo amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha maeneo ya ikolojia, misitu yanatembelewa ili kuweza kuionyesha dunia vivutio vilivyopo sambamba na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kutangaza utalii katika nyanja zote.

"Tumeshiriki katika maonyesho haya ya Afrika Mashariki ili kuionesha Afrika Mashariki na dunia mambo tuliyokuwa nayo sisi kama wakala wa huduma za misitu Tanzania,"amesema Prof.Silayo

Ameongeza kuwa nchi za Afrika Mashariki zinaegemea sana utalii wa wanyama pori lakini kwenye utalii wa Ikolojia haujapewa nafasi kubwa na TFS inataka wananchi watembelee na waone bainoyuwai zilizopo na hata kugusa maeneo hayo.

Profesa Silayo ameyataja baadhi ya maeneo yatakayo tembelewa katika ofa hizo ni pamoja na Bagamoyo ngome kongwe, Kaole lakini pia misitu ya mikoko, misitu ya pugu, panzi wenye bendera ya Taifa na kuwataka watanzania pia kutumia fursa hiyo.

Pia amewaomba wananchi wa Arusha kujitokeza kutumia fursa hiyo ambapo wataenda ziwa duluti na kutembelea misitu ya mlima Meru ambapo ofa hizo zitaisha tarehe 16 na kama kuna ambao hawakuweza kufanya utalii huo kutokana na sababu mbalimbali basi wawasiliane na TFS ili kupata utaratibu mwingine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: