Mkurugenzi wa shule ya St Anne Marie Academy Dk. Jasson Rweikiza akilishwa keki na mmoja wa wahitimu wa shule ya awali wakati wa mahafali yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule ya awali St Anne Marie Acaemy wakicheza wimbo wa Saida Kalori wa chambua kama karanga wakati wa mahafali yao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya St Anne Marie Academy wakionyesha umahiri wao wa kucheza nyimbo za bongo flavor wakati wa mahafali ya shule ya awali yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule ya awali wakiimba nyimbo mbalimbali kwenye mahafali hayo
Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Joyce Chamuhuo, ambaye ni mkuza mitaala wa Taasisi ya Elimu (TIE), akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa shule ya awali St Anne Marie Academy

Na Mwandishi Wetu
SHULE ya St. Anne Marie Academy imesema mpango wake ni kuhakikisha siku moja inashika nafasi ya kwanza kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza, ameyasema hayo leo Oktoba 24,202o wakati wa mahafali ya 19 ya shule ya awali yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

Amejsema ana uhakika watafikia lengo hilo kwani uwezo huo wanao kutokana na rekodi nzuri waliyonayo na walimu mahiri wanaojituma na ambao wamekuwa wakiipaisha kitaaluma.

Amesema shule hiyo imekuwa ikiingia kwenye shule 10 bora kitaifa kwa miaka mingi na wanafunzi wake kuingia kwenye 10 bora kitaifa hivyo hawaoni kikwazo cha shule hiyo kushika namba moja kitaifa.

“Tumeshakuwa wanane kitaifa, wa 13, wa sita, wa 10 sasa kwetu sisi nafasi iliyobaki ni kushika namba moja tu na kwa kweli uwezo huo tunao kwa sababu tuna uzoefu wa kutosha na walimu wenye ujuzi na marifa ya kutosha,” amesema Dk. Rweikiza

Aidha dk. Rweikiza ametangaza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye atarudishwa nyumbani baada ya mzazi wake kufariki na kushindwa kulipa ada.

“Kwa mwaka huu pekee wazazi 40 wameshafariki lakini watoto wao wote wanaendelea na shule hakuna hata mmoja ambaye amefukuzwa. Tumeona tufanye hivi kwasababu baada ya mzazi au mlezi kufariki watoto wanahaingaika sana,” amesema Dk. Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijinini (CCM).

Vile vile, Dk. Rweikiza ameksema St. Anne Marie Academy imeweka mpango kabambe wa kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi katika michezo mbalimbali na sanaa.

Amesema mbali na kuendelea kufanya vizuri kitaaluma wameona ni vyema wakaanzisha mpango huo ili kuwaibua wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kama kuimba, kukimbia, kucheza mpira na vipaji vingine ambavyo wanafunzi wengi wa shule hiyo wameonyesha kuwa navyo.

“Mwanafunzi anaweza kuwa wa kawaida kwenye masomo lakini ana kipaji ambacho kiwapo kiytaibuliwa na kuendelezwa anaweza kufika mbali sana tunaweza kupata waimbaji wa kimataifa,” alisema Rweikiza ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM).

Kwa upande wake Joyce Chamuhuo, mkuza mitaala wa Taasisi ya Elimu (TIE) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, amesema kuna umuhimu kwa shule mbalimbali kutenga angalau siku mbili za kuibua vipaji vya wanafunzi kwenye nyanja mbalimbali na kuviendeleza .

Amewataka wazazi nao kuwa na kamawaida ya kuwafundisha lugha za makabila watoto wao ili kuendeleza tamaduni zao kwani baadhi yao hawajui hata kusalimia kwa kutumia lugha za nyumbani.

“Nimefurahi kusikia Mkurugenzi anasema wameweka mpango wa kuibua vipaji na kuvikuza, hili ni jambo zuri sana na nyinyi shule binafsi mnaliweza sana hili kwasababu mna muda mrefu wa kukaa na wanafunzi hawa,” amesema

“Mkurugenzi amesema hapa kwamba mwanafunzi anaweza asiwe mzuri sana kwenye masomo lakini akawa na kipaji cha kuimba au kucheza na kikiibuliwa na kuendelezwa kinaweza kumfikisha mbali tengeni muda wa kutekeleza jambo hili,” amesema
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: