Timu ya KMC FC imefanya maandalizi yake ya mwisho leo kuelekea katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC soka Tanzania bara hapo kesho Oktoba 18, 2021 dhidi ya Yanga utakaopigwa saa 16:00 jioni katika Dimba la Majimaji Songea mkoani Ruvuma.

KMC FC ambao niwenyeji wa mchezo huo, tayari wamekamilisha maandalizi na kwamba kikosi hicho sasa kipo tayari katika mtanange huo na kuhakikisha kuwa inapata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kuondoka na alama tatu katika uwanja wa Majimaji.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni ambayo iliwasili Oktoba 15 imekuwa na wakati mzuri wakufanya mandalizi tangu ilipokuwa Jijini Dar es Salaam na hata ilipowasili Songea na kwamba hadi sasa wachezaji wapotayari kwa mchezo huo na hivyo kuhakikisha kwamba inapata ushindi dhidi ya wapinzani Yanga.

KMC FC chini ya kocha mkuu John Simkoko na wasaidizi wake Habibu Kondo, Hamad Ally inatambua ushindani uliopo katika mchezo huo lakini wachezaji ,benchi la ufundi wamejidhatiti vizuri kuwakabili wapinzani na hivyo kufanikisha kuondoka na alama tatu muhimu.

“Naweza kusema Ligi ni ngumu na inaushindani mkubwa kwa kila Timu unayokutana nayo, lakini KMC FC tumekuwa na maandalizi mazuri na kwamba yamekamilika kwa asilimia kubwa tangu tulipokuwa Dar es Salaam, kwasababu mchezo huu ulikuwa unafahamika kuwa upo kwenye tariba ya michezo yetu kwa mujibu wa Bodi ya Ligi, hivyo tumejipanga kushinda.

Kikubwa mashabiki zetu wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kuwapa sapoti wachezaji wetu, mechi ipo ndani ya uwezo wetu, KMC FC tumekuja Songea kutoa burudani ya kipee na kwakulitambua hilo tunakwenda kupambania alama tatu , sisi ndio wenyeji wa mchezo hivyo kila kitu tumekamilisha vizuri kuanzia upatikanaji wa Tiketi bila kuwepo kwa changamoto yoyote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: