Katika kukuza na kuenea kwa Lugha ya Kiswahili duniani yatupasa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha lugha hii adhimu inafika mbali.
Serikali imejidhatiti kueneza lugha ya Kiswahili duniani ikiwemo na kuifanya kuwa lugha rasmi kwenye nchi za Ukanda wa Kusini mwa Jangwa La Sahara (SADC).
Watanzania wameaswa kutumia fursa wanazozipata kufundisha Lugha ya kiswahili kwa wageni wa mataifa mbalimbali ili kukieneza kwa kasi pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Akiwa katika majukumu yake ya kikazi, Askari polisi wa Tanzania anaeshiriki ulinzi wa Amani katika nchi ya kidemokrasia ya Congo Ally Babu, amekuwa akitumia muda wa ziada baada ya kazi kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake vya utalii.
Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza lugha ya kiswahili na amekuwa akifundisha walinzi wa amani wenzake kutoka nchi mbalimbali duniani lugha ya kiswahili na wamekuwa wakivutiwa kujifunza kwa wingi.
Babu katika kuutangaza Utalii na vivutio vyake anatumia lugha za kiingereza na Kifaransa kwani wengi wa walinzi wa amani hutoka nchi mbalimbali duniani na kuwatafsiria kwa Kiswahili.
Babu anatumia fursa hiyo kwani ni njia moja wapo ya kuitangaza Tanzania na ujumbe kufika pembe zote za dunia.
Katika kufanikisha harakati hizo za kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili na kutangaza Vivutio vya Utalii, Babu amechapisha picha za maeneo mbalimbali ya utalii kama Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro na Zanzibar.
Maeneo hayo yamekuwa kivutio kwa wageni wengi, na akiwaelezea kwa upana zaidi ili kuwavutia wageni kutembelea vivutio hivyo vya Tanzania.
Tayari wageni wengine wameshaanza kuthibitisha kufika nchini Tanzania kwaajili ya utalii na familia zao.
Askari polisi wa Tanzania anaeshiriki ulinzi wa Amani katika nchi ya kidemokrasia ya Congo Ally Babu akifundisha lugha ta kiswahili kwa walinzi wa amani wenzake kutoka nchi mbalimbali duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: