Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Alex Gashaza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe. Luteni Kanali Michael Mtenjele wakielekea kukagua shamba la miti lililopandwa na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia utaratibu wa Miradi ya Ajira ya Muda katika Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara mkoani Kagera.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akicheza ngoma na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini alipowasili katika Kijiji cha Murugina wilayani Ngara kukagua utekelezaji wa miradi ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: