Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism' ili waweze kuandika kwa weledi habari zinazohusu utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.

Mafunzo hayo ya Waandishi hao wa habari mitandaoni yanafanyika jijini Dodoma kwa muda wa siku mbili Julai 17,2019 hadi Julai 18,2019 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mradi huo unatekelezwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha, Claud Gwandu akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania  kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism'. Picha zote na Kadama Malunde na Albert G. Sengo
Mwezeshaji katika mafunzo ya Uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akitoa mada wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV).
Mwezeshaji katika mafunzo ya Uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akisikiliza hoja kutoka kwa Mshiriki wa mafunzo hayo,William Bundala wa Kijukuu blog wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV).
Washiriki wa mafunzo hayo wakioneshana kitu kwenye Laptop
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika mafunzo kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism'. Picha zote na Kadama Malunde na Albert G. Sengo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: