METHALI - PROVERB
=================

KIHA (Tanzania tribe / Kabila ya Tanzania)

" Akereye inkebhe, mdangi amar irobhe "

ENGLISH (United Kingdom)

" A little of what you fancy does good "

KISWAHILI (Tanzania)

" Kipendacho moyo ni dawa "

====== TANZANIA ======

Katika MAISHA kila mtu ana kitu moyo wake unapenda, mara nyingine ama kwa kujua ama kwa kutokujua wengine wamekuwa hawaitendei haki MIOYO yao kwa kusikia / kusukumwa na sauti za nje (walimwengu).

Ukiona :

- Mtu ana maisha aina fulani mpotezee / jifunze / mshauri

- Mtu anakula mboga mboga badala ya Kuku, Bata na vile vitu vya Kontena na kwa mama Kamche... mpotezee / jifunze / mshauri

- Mtu anatumia Siemens C 25 (Zilipendwa) kama ya kwangu... mpotezee / jifunze / mshauri

Wakati mwingine tunachosha MISULI YA UBONGO kufikiri HASI kuhusu WATU na VITU badala ya kutumia muda mwingi wa thamani kwa kufikiri juu ya MAJIBU YA MATATIZO / CHANGAMOTO za Dunia ambazo kwazo waweza kuzigeuza FURSA zitakazokupelekea kukamata MSHIKO (PESA / UTATUZI wa Changamoto).

Siku moja Mwaka 1996 kama sikosei nilimtembelea Baba yangu Mdogo Mr. Canaan Msigwa nyumbani kwake alipenda kupiga Kaseti ya wimbo KIPENDA ROHO hula nyama mbichi... ule msemo ulinikaa siku zote na kunifanya wakati wote niusikilize kwanza MOYO wangu (Mtu wa Ndani yangu) kabla ya watu wa nje.

Songa mbele

Jiamini

Jithamini

Jitambue

========== ASANTE =========

@ BAGATECH

Godwin D. Msigwa
Qingdao
China
23 April 2019
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: