Madaktari Bingwa wa MOI kwa Kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Zydus wakifanya upasuaji mgumu wa kupandikiza nyonga bandia katika vyumba vya upasuaji MOI.
Madaktari Bingwa wa MOI kwa Kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Zydus wakifanya upasuaji wa mgongo kwa njia ya kisasa katika vyumba vya upasuaji MOI.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa wa hospitali ya Zydus bwana Himanshu Sharma akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika vyumba vya upasuaji MOI.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika vyumba vya upasuaji MOI kwenye kambi ya upasuaji wa Nyonga na Mgongo inayofanywa kwa ushirikiano kati ya MOI na hospitali ya Zydus ya India.

NA KHAMISI MUSSA.

Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na hospitali ya Zydus ya nchini India kuanzia leo Feb 14 na 16, 2019. zitaendesha kambi maalum ya upandikizaji wa nyonga bandia na upasuaji wa Mgongo kwa njia ya kisasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema Katika kambi hii Madaktari bingwa wa MOI na Zdyus. 

watashirikiana kufanya upasuaji mgumu wa kupandikiza Nyonga bandia pamoja na upasuaji wa mgongo kwa njia ya kisasa lengo. ikiwa ni kuwajengea uwezo madaktari bingwa wa MOI ambapo zaidi ya wagonjwa 6 watafanyiwa upasuaji.

“Huu ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Taasisi yetu ya MOI na hospitali hii ya Zydus ya nchini Indi, awali. tulishirikiana katika kliniki maalum na safari wamekuja kwenye kambi hii ya upasuaji, naamini madaktari Bingwa wetu 

Watapata mbinu mpya na za kisasa ili waendelee kutoa huduma hizo hata baada ya wageni hawa kuondoka” Alisema Dkt Boniface.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Uhusiano wa kimataifa wa hospitali ya Zydus, Himanshu Sharma amesema ushirikiano kati ya MOI na Zydus umekuwa wenye mafanikio makubwa toka mwaka jana ambapo wagonjwa wamekuwa wakinufaika kwa kupata huduma kwa kutumia mbinu za kisasa bila ya kusafiri kwenda nje ya nchi.

“Tunafurahi kwamba tumepata fursa ya kuwapatia mbinu mpya na za kisasa za upasuaji wenzetu hapa MOI, teknolojia na mbinu za upasuaji zinabadilika kila siku na kwakuwa tunashirikiana, wataalamu wetu wameleta mbinu mpya ambazo tunazitumia kule  India, lengo ni kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma kwa mbinu na teknolojia bora hapahapa Tanzania” alisema Bwana Sharma

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Mifupa wa MOI aliyebobea kwenye upandikizaji wa Nyonga bandia Dkt Violeth Lupondo amsema mbinu wanazopata zitawasadia kuendelea kutoa huduma hizo hata baada ya madaktari kutoka Zydus kuondoka.

“Huwa tunafanya kila siku aina hizi za upasuaji lakini huu wa leo ambao tunafanya na wenzetu kutoka Zydus ni wa tofauti na mgumu, tunajifunza mambo mengi kutoka kwao na wao pia wanajifunza kutoka kwetu, ni matarajio yetu wagonjwa wengi zaidi watanufaika” Alisema Dkt Lupondo

Hii ni sehemu ya Mkakati wa Taasisi ya MOI wa kuhakiklisha huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa nchini na kwa  teknolojia ya kisasa sawa na ile inayotumika kwenye mataifa yalioyoendelea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: