Rais wa zamani wa Marekani George H W Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94, mwanawe rais wa zamani pia George W Bush ametangaza.

George Bush Senior, kama alivyofahamika sana, alifariki dunia mwendo wa saa nne na dakika kumi usiku (saa kumi na dakika kumi GMT), msemaji wa familia hiyo ametangaza.

Alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1993 baada ya kuongoza kwa mihula miwili kama makamu wa rais chini ya Rais Ronald Reagan.

Aprili, alilazwa hospitalini akiwa na maambukizi kwenye damu lakiniakatibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

George Herbert Walker Bush amefariki miezi saba tu baada ya kifuo cha mke wake Barbara.

Viongozi wamekuwa wakituma salamu za rambirambi na kumkumbuka mwanasiasa huyo, wakiongozwa na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump aliyemsifu kwa "uhalisiwa wake, ucheshi na kujitolea kwake kudumisha imani, kwa familia na kwa taifa.

Bendera katika ikulu ya White House zitapepea nusu mlingoti huku mipango ya mazishi ikiendelea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: