Imekuwa kawaida Kwa jamii ya kitanzania kushiriki na watoto wanaolelewa katika vituo vya watoto wenye uhitaji chakula na mahitaji mengine hususan katika msimu wa sikukuu.

Mwananchi mmoja mmoja , vikundi taasisi na ofisi mbalimbali za serikali na binafsi zimekuwa zikitoa msaada wa chakula na mahitaji mengine kwa vituo vya watu wenye uhitaji lakini je umeshawahi jiuliza watoto hao wanahitaji nini zaidi?

“Mimi napenda sana mtu akipeleke kuogelea lakini, Sisi tunataka kutoka na kujumuika na watu wengine tucheze nao na tufurahi badala ya wao kuja kutuachia chakula tuu nakuondoka “ alisema Mudy Mbeki mtoto anayelelewa katika kituo cha Yatima Group Trust Fund chamazi ambaye alikuwa akisherehekea sikukuu ya krismass ikiwa ni maadhimisho ya wakisto ulimwenguni kote wakikumbuka kuzaliwa kwa mesihi Yesu Kristu.

Mudy ni mmoja kati ya watoto zaidi ya 250 kutoka vituo viwili vya watoto wenye uhitaji vya Yatima Group Trust Fund Chamazi na Kurasini Orphanage Center waliokutanishwa pamoja katika ukumbi wa kifarahi katika hoteli ya The Dar es salaam serena Hotel kusherehekea na wafanyakazi pamoja na wadau wa serena msimu huu wa sikukuu.

“Tumekodi zaidi ya magari matano (5) kwenda kuwafata watoto katika vituo vyak Kurasini na Chamanzi ili wawalete watoto hapa Serena Hotel tufurahi nao sikukuu hii, na huu ni utamaduni wetu wa miaka mingi baada ya kugundua watoto wanatakq sana kutoka nje ya makazi yao waliozoea kipindi hiki cha sikukuu” alisema Sophia Mketo Meneja Rasilimali watu wa Hoteli ya Serena.

Aliongeza kuwa sherehe hiyo wameshirikiana na wadau wa serena kwa kuwanunulia zawadi watoto wote waliofika hapo kwenye sherehe na lengo kuu ni kuhakikisha watoto wanakuwa na furaha na kuona wanathaminiwa.

Amesema hapo awali walikuwa wakipika chakula na kupeleka vituoni lakini watoto hao ndio walioonesha hamu ya kutaka kutoka nje ya vituo ndipo walipoanza utamaduni wa kuwatoa outing na imeendelea hivyo kwa miaka 3 mfululizo sasa.

Pamoja na kuwaandalia chakula cha mchana, zawadi na michezo mbalimbali serena Hoteli ilimualika Mchekeshaji maarufu Stan Bakora ambaye naye aliwaelezea watoto historia ya maisha yake kuwa akiwa mdogo pamoja na wadogo zake wawili walifiwa na wazazi wao na walilelewa na bibi yake ambaye baada ya miaka kadhaa naye alifariki na hivyo Bakora kuchukua jukumu la kuwalea wadogo zake kwakutumia kipato alichopata kupitia sanaa yake ya uchekeshaji.

Mbali na kuwachelesha na kuimba na watoto hao waliokuwa na sura za furaha aliwakaribisha wanajamii wote kuwasiliana naye iwapo watataka ajumuike na watoto yenye uhitaji siku yeyote. “ mimi ni yatima kama nyinyi lakini nina ndoto kubwa na namshukuru Mungu kidogo naweza kujimudu na kusomesha wadogo zangu hivyo msikate tamaa na iwapo kuna yeyote atataka kunitumia kushiriki na watoto kama leo walivyofanya serena nawakaribisha tuwasiliane” .

Naye katibu mtendaji wa kituo cha kulelea watoto cha Yatima group Trust Fund Chamazi, Fred Njegeja ameshukuru wanajamii kwa mchango wanaoutoa katika kituo hicho na kuwaomba kuzingatia hitaji la watoto kutoka nje ya kituo na kujichanganya na wanajamii katika kusherehekea sikukuu.

“Hapa kituoni kwetu asilimia 95 ya msaada unatoka kwa wanajamiii na wanakuja sio tuuu kipindi cha sikukuu lkn na wakati mwingine tuu waki wiwwa kutoa msaada kwa watoto katika kituo chetu, lakini kipindi hichi cha likizo ni vyema hata mwenye uwezo wa kuchukua watoto 5 akatoka nao outing inawasaidia sana wanakuwa wanafurahi na kuona wanathaminiwa.”

Amesema hali ya kutoka nao nje ya maeneo ya kituo ni kitendo kizuri kwakuwa watoto wengi katika kituo hicho ni wale ambao wamefukuzwa makwao au wazazi wao wamefariki hivyo wamejijenga katika fikra ya kuwa hawapendwi, hivyo kuwachukua kucheza nao na kushiriki nao chakula nje ya makazi yao kunaongeza sana morali na kuona yakuwa wanathaminiwa.

Mbali na chakula pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa Watoto Njegeja amesema wapo wanajamii ambao hujitolea kupeleka michezo mbalimbali na kuburudika na watoto pamoja lakini kama jamii itajitokeza kufanya kama kilichofanywa na serena Hoteli ni dhahiri itabadili kwa kiasi kikubwa mtazamano wa watoto hao wanaolelewa katika vituo vya watoto yatima
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: