Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Hamza Johari.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Shirika la Ndege la Fastjet linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni Sita na Mamlaka zinazotoa huduma ya usafiri wa Anga pamoja na Wasambazaji, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Hamza Johari amesema.
Bw. Johari ameweka bayana kuwa shirika la Fastjet lina matatizo makubwa yanayofanya lisiendelee kutoa huduma ya usafiri wa anga. Amesema kuwa walivyotoa siku 28 ya kufunga huduma za shirika hilo walikuwa wamejiridhisha kutokana na madeni ya shirika hilo pamoja na kumiliki Ndege ambayo haina uhakika wa kufanya safari za anga.
Johari amesema kuwa shirika hilo lilikuwa linamilikiwa na Mwingereza na baada ya kuondoka wazawa wakanunua hisa akiwemo Mwenyekiti Mtendaji wa shirika hilo Laurence Masha ambao walianz kuanza kuendesha shirika hilo.
Aidha ameeleza kuwa baada ya kupata matatizo hayo Meneja Usimamizi wa Ndege hizo alijiuzuru na ndiye aliyekuwa anajua masuala ya Ndege hivyo Mamlaka haiwezi kuruhusu Ndege kuruka bila kuwepo kwa mtu huyo.
Aidha amesema kuwa taarifa ya kuleta Ndege zilizotolewa na Mwenyekiti Mtendaji Laurence Masha Desemba 22 mamlaka ilikuwa haina taarifa badala yake taarifa imewafikia Desemba 24 na bado wanaifanyia kazi.
Pia amesema kuwa moja ya masharti waliyowapatia ilikuwa ni kupatikana kwa Meneja mwenye utaalamu wa masuala ya Anga ambapo Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet Laurence Masha alimteua Meneja wa Shirika hilo Laurence Masha kuwa Meneja usimamizi.
Johari amesema sharti lingine ilikuwa ni kuandika andiko la biashara ikiwa upatikanaji wa fedha za uendeshaji wa Shirika. Mkurugenzi Mkuu huyo wa TCAA amesema kuwa kuzuia kwa shirika hilo kufanya biashara ya usafiri wa Anga ni kuipendelea ATCL ni maneno tu kinachotakiwa kwa kila shirika kufuata sheria zilizowekwa kwa ajili ya Usalama wa abiria wanaotumia usafiri wa anga.
"Hakuna ugomvi shirika la Fastjet kufuata matakwa ya sheria kwa maslahi mapana ya abiria pamoja na kulipa madeni" amesema Johari.
Toa Maoni Yako:
0 comments: