Afisa wa Polisi kutoka Dawati la jinsia Mkoa wa kipolisi Kimara Afande Anna Mihayo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wanaharakati wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS)

Jeshi la polisi nchini kwa kushirikiana na asasi za kiraia zinazotetea haki na maslahi ya watoto na wanawake zimetakiwa kuhakikisha zinasambaza elimu katika kata zote, ikiwemo kufanya makongamano pamoja na kutoa matangazo kwa wingi kwenye Tv na redio ili wananchi wajua madhara ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Hayo yameelezwa mapema wiki hii jijini Dar es salaam na Afisa wa polisi kutoka Dawati la jinsia Mkoa wa kipolisi Kimara Afande Anna Mihayo wakati akitoa elimu kwa wanaharakati wa GDSS kuhusu nafasi ya mwananchi katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kupitia Dawati la Jinsia.

Afisa huyo amesema kuwa ili kufanikisha jambo hili ni vema wananchi kushirikiana kwa pamoja na jeshi la polisi kwa kuweza kuwafichua watekelezaji wa ukatili huo kwa kuwa ni watu tunaoishi nao katika maisha yetu ya kila siku.

Aidha ameongeza kuwa zipo mbinu mbalimbali ambazo wananchi wanaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza kama sio kulimaliza kabisa tatizo hili moja wapo ikiwa ni kutumia waandishi wa habari ili kuweza kusambaza habari kwa jamii na vyombo husika vitasikia na kuweza kuchukua hatua stahiki.

Wanaharakati wa semina za GDSS wakifuatilia semina kwa makini.

Aliendelea kusema kuwa mpaka leo hii bado kuna baadhi ya wananchi wanaogopa kutoa taarifa polisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uoga wa kuongopa kituo au kuogopa kujenga uhasama na majirani au ndugu.

“Wananchi wengi wanakuwa na taarifa muhimu za watu wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia kwa kuwa mara nyingi watekelezaji wa mambo haya wanakuwa ni ndugu wa karibu au majirani, hivyo walio wengi uogopa kupewa ubaya na familia au jirani, basi watu wananyamaza kimya mpaka tatizo linapokuwa kubwa kama muhanga kuuwawa au kujeruhiwa vibaya ndipo wanakuwa tayari kuongea ukweli”. Alisema Afande Anna

Lakini pia baadhi ya wanaharakati wamelalamikia swala la rushwa katika vituo vya polisi kwa kusema kuwa baadhi ya polisi wakipewa fedha na muhusika wa utekelezaji wa ukatili huo wanaamua kufuta kesi kwa madai kuwa muende mkayamalizie nyumbani bila mtuhumiwa kuchukuliwa hatua yeyote.

Kwa upande wake Mwanaharakati Nyanjura Kalindo alisema kuwa jambo hili bado ni gumu kutokana unapeleka kesi polisi ya mtoto aliyebakwa na mlezi wake kesi ikifika kule polisi Yule mlezi akifungwa na huyu mtoto huku anakosa msaada na pia familia inachukua hatua ya kumtenga Yule mtoto na kugoma kumpa mahitaji yake muhimu kwa kuwa amesababisha kufungwa kwa ndugu yao.

Semina ikiendelea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: