Bw.George Mwimbe akitoa malalamiko yake kwa waandishi wa habari (hawapo picha) katika mtaa wa Ndaji Jijini Dodoma ili Serikali iweze kuwasaidia kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati yao na watu waliovamia siku za karibuni
Mauld Kambi akizungumza na waandishi wa habari pamoja wananchi wa mtaa wa Ndaji ulipo mkoa wa Dodoma huku akiomba msaada kwa Serikali iwasaidie katika kupata haki yao baada ya kuingia kwenye mgogoro wa ardhi baina yao na watu walioibuka hivi karibuni.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Ndaji mkoani Dodoma wakiwa na mabango yao wakiomba msaada kwa Serikali baada ya kuvamiwa na watu katika ardhi yao.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Ndaji wakionesha mabango yao kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Bi.Foibe Sabuni akionesha sehemu ya ardhi yake ambayo kwa sasa anaambiwa kuwa ni mvamizi katika mtaa wa ndaji uliopo mkoani Dodoma baada ya kuibuka mgogoro wa ardhi baina yao na watu walioibuka katika maeneo hayo
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa ndaji jijini Dodoma wakiwa wamekusanyika kwa waandishi wa habari wakitoa malalamiko yao baada ya kuibuka mgogoro wa ardhi ulioibuka hivi karibuni
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akitolea ufafanuzi kuhusu mgogoro wa ardhi uliopo katika mtaa wa ndaji

Na.Alex Sonna,Dodoma

Wakazi zaidi ya 300 wa mtaa wa Ndaji Jijini Dodoma wamemuomba waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kuingilia mgogoro wa ardhi ulipo baina yao na watu ambao wameibuka hivi karibu kudai kuwa ndiyo wamiliki harali wa maeneo hayo na kutaka kuwahamisha wazawa.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo kwa nyakati tofauti walidai kuwa mgogoro huo kama hauta tatuliwa haraka upo uwezekano wa kutoa kwa machafuko.

Mmoja wa wakazi hao George Mwimbe, amesema kuwa hivi karibuni wameibuka watu kutoka katika maeneo mbalimbali wakitaka kuwahamisha kwa madai kuwa wao ndiyo wamiliki harali wa maeneo hayo.

Amesema kuwa wanashangaa kuona watu hao ambao wameibuka hivi karibu kudai kuwa wanazohati za umriki wa maeneo hayo na kuwataka waondoke huku wakitumia vyombo vya usalama kuwatisha.

“Hivi sasa watu wanakamatwa na kuwekwa ndani bila kukosa na tunashangaa kuona jeshi letu la polisi kushirikiana na hawa watu ambao wanataka kutupokonya haki yetu”amesema Mwimbe

Mwimbe amesema kuwa wao ni wazaliwa wa maeneo hayo na wazazi wao ndio walikuwa wamiliki wa maeneo hayo lakini wanashangaa kuona hivi karibu mara baada ya Rais kutangaza jiji watu wametoka maeneo mbalimbali na kutaka kuwatapeli maeneo yao.

Hata hivyo amesema kuwa kutokana na hali hiyo wanaiomba serikali kuingilia kati mgogoro huo kwani hivi sasa wamekuwa wakitishiwa maisha na watu hao ambao ni matajiri kuliko wao.

Kwa upande wake Bakari Kambi amesema kuwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa upo uwezekano wa kutokea kwa machafuko kwani washachoka kuonewa bila kupatia msaada wowote.

“Hivi sasa tumechoka hatuwezi kuendelea tena kuvumilia kuonewa tupo tayari kwa lolote hata kama kufa tupo tayari hatuwezi kuendelea kuona wazazi wetu wanasumbuliwa na watu wakuja wakati sisi ndiyo wenye maeneo”amesema

Akizungumzia juu ya malalamiko Mkurugenzi mtendaji wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi,amesema kuwa mgogoro huo wanaufahamu na upo katika makundi tofautitofauti na wanaangalia njia sahihi ya kuweza kuutatua.

Kunambi amesema kuwa wanaangalia namna ya kulinda haki ya kila mtu kwa kuja na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kutumia wataalamu mbalimbali wa ardhi ili kila kundi lipate haki yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: