Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akaunti ya akiba ya wanawake inayoitwa LULU iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukimbi wa Kisenga Makumbusho jijini Dar es salaam, LULU ni akaunti mahsusi kwa mwanamke anaejua malengo yake ya kimaisha iliyoanzishwa na AccessBank Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Jokate Mwegelo akiwa jukwaani mara baada ya kuwasili ukumbini kutoka kulia ni Bi. Maida Waziri Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Constructiors Limited, Grace Metta kutoka AccessBank Tanzania na kushoto ni Jennifer Bash Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Alaska Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa AccessBank Tanzania Bw.Armando Massimiliano Sirola akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Akaunti ya Lulu iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Kisenga jijini Dar es salaam.
Bi. Maida Waziri Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Constructiors Limited akitoa mada wakati wa uzinduzi wa akaunti hiyo.
Namala Rwebandiza MC wa uzinduzi huo akizungumza na waalikwa.
Baadhi ya wafanyakazi wa AccessBank Tanzania wakiwa katika uzinduzi huo
Grace Metta Company Cecretary kutoka AccessBank Tanzania akizungumza na akina mama na akina dada waliofika kwenye uzinduzi wa akaunti ya LULU.
Jennifer Bash Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Alaska Tanzania akitoa mada kwa akina mama waliofika kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Huduma AccessBank Tanzania Bw.Andrea Ottina akigawa fulana kwa akina mama waliokuwa tayari kufungua akaunti ya LULU wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya akina mama na akina dada waliofika kwenye uzinduzi wa akaunti ya LULU iliyoanzishwa na AccessBank Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Kisenga jijini Dar es salaam.
Katika kuendelea kuwajali wateja wake AccessBank Tanzania imezidi kuboresha huduma zake, kwa kuongeza akaunti ya akiba ya wanawake inayoitwa LULU . Akaunti hii ilizinduliwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo jumamosi tarehe 10 Novemba 2018 ukimbi wa Kisenga International Conference Centre.
Akizungumza katika uzinduzi huo DC Mwegelo amesema "LULU ni akaunti mahsusi kwa mwanamke (anaye jithamini) anaejua malengo yake ya kimaisha, anaeona mbele na kupanga kwa ajili ya baadae yake. Akaunti hii imebuniwa ikiwa na mpango mzuri wa kujiwekea akiba na kumfanya mwanamke kutimiza malengo yake, hivyo kumsaidia kusonga mbele kiuchumi".
Mh. Jokate Mwegelo amesema LULU ambayo ni maalumu kabisa kwa mwanamke. ni akaunti maalum kwa akina mama na pia itakua mkombozi kwao kwani wanawake waliowengi wataweza sasa kujiwekea akiba kwa muda maalumu hivyo kusaidia kutimiza malengo waliyojiwekea.
Lengo la akaunti hii ni kumwezesha mwanamke kufikia malengo yake,kama tunavyojua mwanamke ndio kila kitu katika jamii na anapofanikiwa na pia Jamii nzima itafanikiwa. Mwanamke anapokua na uwezo wa kutatua matatizo yakifedha, basi familia au Jamii husika inakua imeondokana na kadhaa nyingi.
Niwapongeze AccessBank Tanzania kwamba moja wapo ya faida ya akaunti hii ni; Mtapata fursa ya kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yatakayokuwa yakitolewa na benki hii kupitia wakufunzi mbalimbali ambao benki itawaandaa kama hawa waliopo leo.
Mwisho kabisa nirudie kuwapongeza tena AccessBank Tanzania kwa kua miongoni mwa mabenki machache nchini yenye huduma maalumu kwa ajili ya Wanawake. Jambo hili linaonyesha jinsi gani Wanawake tulivyo na umuhimu katika Jamii yetu. Baada ya kusema hayo machache, basi nitangaze rasmi kwamba akaunti hii ya LULU imezinduliwa rasmi leo hii siku ya Jumamosi, tarehe 10 November 2018
Akizungumzia maendeleo ya Akaunti hiyo Mkuu wa Idara ya Opereshani wa AccessBank Tanzania Ndugu Andrea Ottina alisema, “AccessBank Tanzania kwa kua miongoni ya Taasisi yakifedha ambayo imekuwa ikiwajali na kuwathamini wananchi, hasa wale wenye kipato cha chini pamoja na wafanya biashara wadogo na wakati, ambao wengi wao wanaonekana kuwa hawana vigezo na hivyo kutengwa na taasisi za kifedha.
Jambo hili AccessBank Tanzania wameliona, na wao kuwa miongoni mwa Taasisi inayowakumbuka na kuwawezesha wananchi wa aina hii kwa kuwaletea huduma zakifedha kulingana na maitaji yao. Na pia haijawaaacha akina mama na vijana wakike ambao miongni mwao wamekuwa wakijihusisha na biashara ndogo ndogo ili kukidhi maisha yao ya kila siku.”
AccessBank Tanzania ni taasisi ya kifedha inayolenga kutoa huduma za kibenki kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia wanahisa wake wa kimataifa ambao ni AccessHolding, International Finance Corporation (Word Bank), KfW, African Development Bank na MicroVest, maono ya benki ni kujidhatiti katika uanzishaji wa mifumo ya kifedha inayochochea maendeleo ya jamii kwa kutoa huduma zilizobora kwa watu wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments: