Yessaya Mwakifulefule (kulia) akiwa na mkewe ambaye kwa sasa ni marehemu Doty Sherry Yessaya.
---
Ndugu Zangu, Asanteni sana kwa support yenu na salam za Faraja Kwangu mimi na binti Yetu Sharon.

Siku kama ya Leo last week SAA mbili asubuhi nliongea na Doroth ( ambae kwa Sasa ni Marehemu) ,japo alilalamika headache siku 2 kabla.Jumamosi ile Doroth alinambia alikua very fine.Nlimwambia ningempigia tena SAA sita mchana kabla sijaenda Ku angalia mpira wa Simba na Mtibwa ktk uwanja wa CCM kirumba.

Saa sita ilipofika namba ya wife ilinipigia nilipopokea hakua yeye Bali ni binti Yetu Sharon (tuna mtoto mmoja mwenye miaka 9) alinambia kani miss (mie naishi mwanza kikazi hivyo aidha mie huja Dar mwisho wa mwezi au wao walikua wakija mwanza)

.nikapiga nae story mbili tatu. kisha nikwamwuliza mama yukwapi.?akasema Kalala.. Nikamwomba ampelekee mama Simu.Ndipo nliposhangaa naongea hiki anajibu kingine (kama ana weweseka)

Nlikata Simu na kumpigia dada wa Kazi ambae alikua Jikoni ,nikamwwmbia akimbie JUU akamwangalie mama..ndio dada aliponza kupiga mayowe kwamba mama kazidiwa.nilikata Simu na kupiga Simu kwa majirani ambao walikuja kummbeba na kumwaisha Muhimbili.. Ambako madktari marafiki zetu ambao nliwatafuta wampokee watusaidie... Nao walijitahidi sana...

Nlifanikiwa kupata Ndege ya usiku kuja dar..ambako nlifikia hosp na kumkuta Dotty hana fahamu bado, hali hii iliendelea hadi Jumapili SAA Tisa alipofariki.

Dotty Simu yake ya mwisho alinambia yupo vema....Bado siamini.

Wengi wenu mmekua mkiuliza imekuaje?maana hamkuwa kusikia akiumwa hivyo mshtuko mlioupata ninyi Rafki Zangu ndio nloupata mie....bado nahisi nipo ndotoni...

Ila salam zenu..zinanipa nguvu.Asanteni kwa Michango yenu sana...asanteni sana.....

Tumemzika Dotty hapa Kyela... Nitarudi Dar Jumanne na Sharon wangu.Ntakua Dar kwa siku kadhaa kabla sijarudi Mwanza.Natakiwa kazini trh 3 sept.

Asanteni Sana.....

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Pole sana kwa msituko mkubwa huo Mungu ni mfariji wetu haachi kutufariji Wana wake

    ReplyDelete
  2. Mungu wetu ni mfariji sana

    ReplyDelete