Mchezaji wa timu ya Portland (Jezi ya Kijani) Denis Babu akijaribu kuwatoka wachezaji wa Mchenga BBall Stars (jezi nyeupe) Cornelius na Chriss wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 uliofanyika mwishoni mwa wiki hii na Portland kufanikiwa kushinda kwa pointi 71 dhidi ya 64 za Mchenga BBall Stars.
Mchezaji wa timu ya Mchenga BBall Stars(jezi nyeupe) Baraka Isack akiambaa ambaa na mpira pembeni ya mchezaji wa Portland wakati wa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Sprite BBall Kings 2018 uliofanyika mwishoni mwa wiki hii na Portland kufanikiwa kushinda kwa pointi 71 dhidi ya 64 za Mchenga
Mashabiki wakiwa wanafuatilia michuano ya Sprite BBall Kings 2018
TIMU ya Flying Dribblers imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kufanikiwa kushinda michezo yake miwili dhidi ya wapinzani wake Team Kiza huku Bingwa Mtetezi Mchenga BBall Stars wakibanwa mbavu na Portland katika mchezo uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Flying Dribblers ambao waliishia hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya mwaka uliopita, wameshinda mechi mbili kwenye 'best of three' za nusu fainali hivyo kukata tiketi ya fainali moja kwa moja.
Kwenye game 1 Flying Dribblers walifanikiwa kushinda pointi 84 kwa 75 za Team Kiza. Katika mechi ya leo nyota wa Flying Dribblers Baraka Mopele amefunga pointi 21 rebound 3 na Assist 1 hivyo kuipa tiketi ya fainali timu yake.
Kwa upande wa Team Kiza mchezaji Abdul Chingwengwe amefunga pointi 23, rebound 5 na Assist 2. Flying Dribblers sasa wanasubiri mshindi wa game 3 kati ya Portland dhidi ya Mchenga Bball Stars ili kujua wanakwenda kuchuana na nani kwenye fainali.
Timu ya Portland imefanikiwa kushinda game 2 ya nusu fainali ya michuano ya Sprite Bball Kings dhidi ya Mchenga Bball Stars hivyo kulazimisha kucheza game 3 ili kupata mshindi atakayekwenda fainali.
Katika mchezo huo uliweza kumalizika kwa Portland kushinda pointi 71 dhidi ya 64 za Mchenga Bball Stars ambao ndio mabingwa watetezi.
Nyota wa Portland Denis Babu ameweza kuifungia timu yake pointi 42, na kuchukua rebound 7 na Assist 2 na kuwaokoa kutoaga mashindano kwenye game 2.
Katika mchezo huo Portland waliweza kucheza wachezaji watano kwa dakika zote 40 bila kuwa na mchezaji wa akiba na kufanikiwa kushinda mechi hiyo.
Kwa upande wa Mchenga Bball Stars wao waliwaeza kuongozwa na nyota Baraka Isack ambaye amefunga pointi 22, rebound 3 na Assist 2, japo zimeshindwa kuisadia timu yake kwenda fainali bila kucheza game 3.
Katika game 1 Mchenga Bball Stars walishinda kwa pointi 70 kwa 54. Portland sasa zitacheza game 3 ili kumpata mshindi atakayekwenda fainali kuwania milioni 10 akiwa bingwa au milioni 3 akiwa wa pili pamoja na milioni 2 kwa atakayekuwa MVP.
Toa Maoni Yako:
0 comments: