NUSU Fainali ya kwanza ya Michuano ya Sprite BBall Kings imefanyika wikiendi hii kwa michezo miwili kupigwa katika Uwanja wa Ndani wa Taifa.
Mchezo wa kwanza ulianza kwa kuwakutanisha Flying Dribblers dhidi ya The Team Kiza ulikuwa na ushindani mkubwa sana kwa timu zote mbili kutafiuta ushindi wa kwanza na ulimalizika kwa timu ya Flying Dribblers kuibuka na ushindi wa vikapu 84 kwa vikapu 75 vya The Team Kiza.
Portland waliwakaribisha Mabingwa watetezi Mchenga BBall Stars katika mchezo wa pili, mechi hiyo iliyokuwa na presha kwa pande zote mbili kuanzia nje ya uwanja huku manahodha wakitambia uliweza kuleta burudani ya aina yake.
Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa mpaka inafikia dakika ya mwisho ya mechi hiyo Mabingwa watetezi Mchenga BBall Stars waliweza kuondoka kidedea kwa vikapu 70 dhidi ya 54 vya Portland.
Nusu fainali ya pili inatarajiwa kuwa wikiendi ijayo ambapo zitawakutanisha tena The Team Kiza akiwa mwenyeji kwa kumkaribisha Flying Dribblers kwa mchezo wa kwanza na Mchenga BBall Stars akiwa mwenyeji dhidi ya Portland.
Katika mchezo huo wa pili, timu itakayoshinda mfululizo itafanikiwa kuingia moja kwa moja katika hatua ya fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 na mshindi wa michuano hiyo atajiondokea na kitita cha Milioni 10, mshindi wa pili akipata Milioni 3 huku mchezaji bora wa michuano (MVP) akibeba Milioni 2.
Michuano hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Sprite pamoja na kituo cha runinga cha EATV na EA Radio ikiwa ni mara ya pili mfululizo
Toa Maoni Yako:
0 comments: