Leo nimekutana na vijana wawili. Wa kwanza amekuja kuomba kazi. Nikamuuliza kazi gani. Akanijibu YOYOTE. 

Nikamuuliza kwa hiyo mimi ndio nikutafutie kazi? Akakosa jibu. Nikaamua kumtembeza kidogo. 

Nikamuuliza tena kazi gani unataka? Akanijibu mimi sijui mna kazi gani. Hakuona kazi anayotaka au anayoweza kufanya. Tukaagana. 

Kijana wa pili yeye amesoma Accounts. Ila hana uzoefu wowote. Akaniambia anahitaji mtu amtrain. Nikamwambia, mimi ni mwanasheria nani alinifundisha kufanya biashara? Akakaa kimya. 

Nikamuonyesha branding. Nikamwambia nani kafanya. Akasema wewe. Nikamuonyesha garden. Nani kaisimamia. Akasema wewe. Nikamuuliza hatuuzi vinywaji? Aksema ndio. Nikamuuliza kwenye sheria kuna kozi ya kuuza vinywaji? Akasema hapana. 

Nikamaliza kwa kumwambia nenda ofisini wakupe meza ufanye kazi. Kama huwezi nenda nyumbani ukasubiri training. Ameenda ofisini. Naamini ataweza. Vijana hawa ni kati ya vijana wengi sana ambao wanateseka kutafuta ajira. 

Wengi hawatapata kwa sababu hawajui jinsi ya kupata ajira. Tatizo ni kubwa. Mfumo wetu wa elimu hauwaandai vijana kulingana na UHALISIA na UKWELI uliopo huku mtaani. 

#TheDon #TheDonsGroup #TheDonsTravels #getangrygetinspired #Maisha #KeshoYako #TouchingLives #Lessons @the_donsgroup please follow us #SalesMan #LetUsServeYouInArusha #Usafiri

Imeandikwa na

Alberto Msando.
@albertomsando.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: