Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob akiongea na wahudumu ya afya jinsi ya kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto katika mafunzo yaliofanyika katika taasisi ya kimataifa ya mafunzo ya afya Ifakara TTCIH wilayani Kilombero Mkoani Morogoro kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi TTCIH Dkt. Edward Amani na kulia ni dakari bingwa wa magonjwa ya akinamama na uzazi Dkt. Hassan Njete kutoka katika HospitaI ya mtakatifu Fransisco Ifakara.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob akifafanua jambo kwa watoa huduma za afya kutoka Zahanati na Vituo vya Afya mbalimbali ambao walikua wanapata elimu juu ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto.
 Watoa huduma za Afya kutoka katika Zahanati na Vituo vya Afya za wilaya za Morogoro wakifatilia kwa makini elimu ya utoaji huduma za dharula kwa mama mjamzito na mtoto mchanga mafunzo yaliofanyika katika Taasisi ya kimataifa ya mafunzo ya Afya Ifakara TTCIH.
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya kimataifa ya mafunzo ya Afya Ifakara TTCIH Dk Edward Amani akifafanua jambo kwa watoa huduma za Afya kutoka Zahanati na Vituo vya Afya mbalimbali ambao walikua wanapata elimu juu ya kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto, mafunzo yaliofanyika katika Taasisi ya Kimataifa ya mafunzo ya Afya Ifakara TTCIH.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob akiteta jambo na Mtafiti mkuu wa mradi Dkt. Angelo Nyamtema anayefuatia ni Dkt. Abdallah Abdallah anetabasamu ni Dakari bingwa wa magonjwa ya akinamama na uzazi Dk Hassan Njete na wa mwisho ni Dkt. Sister Nathalia Makunja ambae ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya akinamama na uzazi kutoka katika HospitaI ya mtakatifu Fransisko Ifakara.
Washiriki 15 kutoka katika Zahanati na 5 kutoka katika Vituo vya Afya kwenye wilaya za Morogoro , Kilosa ,Gairo na Mvomero wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma za Afya ikiwa na lengo ya kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Na Mwandishi Wetu.

Watoa huduma wa afya wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepukan na vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ili kuhakikisha takwimu za vifo vya akina mama wajawazito haziongezeki kama ilivyo sasa kwani takwimu zinaonyesha vifo vya akina mama vimeongezaka kutoka 454 katika vizazi hai laki moja kwa mwaka jana hadi kufikia vifo 556 kwenye vizazi hai laki moja. 

Rai hiyo imetolewa na mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Frank Jacob katika mkutano wa kuwajengea uwezo watoa huduma za Afya kutoka Zahanati na Vituo vya Afya 20 Mkoani Morogoro ambapo amesema ili kupunguza vifo vya akina mama wajawazito nilazima wataalamu wa Afya wafate vigezo vya utoaji wa huduma bora kama kuangalia madhurio ya akima mama Clinic, kutoa dozi ya pili (ASP) ya kukinga Maralia , Madini ya chuma na Folic Acid kwa mjamzito pamoja na kutoa elimu kuhusu uzazi wa mpango ambao pia hupunguza vifo vya akina mama kwa asilimia 44. 

Mafunzo hayo ambayo yanatoa nafasi kwa watoa huduma kutoka katika Zahanati na Vituo vya Afya kuweza kutoa huduma za dharula kwa mama mjamzito na mtoto wamebaisha changamoto mbalimbali ikiwemo ya jinsi ya kutoa huduma kwa mama wenye vifafa vya mimba na wale ambao wanatokwa damu nyingi baada ya kujifungua huku tatizo la usafiri vijiji nalo limeonekana kuwa sehemu ya changamoto.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: