Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.
Ikiwa imebaki siku moja kuanza kwa Michuano ya Kombe la Dunia nchini Russia, Timu ya taifa ya Hispania rasmi imetangaza kumfuta kazi Kocha wake, Julen Lopetegui kama Kocha Mkuu wa kikosi hicho.
Spain rasmi imemfuta kazi Kocha huyo ndani ya Masaa 24 kabla yakuanza Kombe la Dunia baada yakushtushwa na taarifa ya Kocha huyo kusaini Mkataba wa miaka mitatu na Real Madrid ya Hispania siku ya Jumanne.
Julen Lopetegui alitangazwa kuchukua mikoba ya Zinedine Zidane mapema wiki hii jambo ambalo lilishangaza wengi.
"Tunatakiwa kuangalia zaidi timu ya taifa inayoshiriki Kombe la Dunia", maneno ya Rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania, Luis Rubiales. "Tumefurahishwa na tulichokipata kutokana na sehemu kubwa ya mchango wake, na lazima tumshukuru na kumtakia mafanikio.
Julen Lopetegui alijiunga na Hispania kama Kocha Mkuu Julai 2016 aliongoza kikosi hicho michezo 20, akishinda michezo 14, na kutoka sare michezo sita.
Hispania itacheza na Portugal siku ya Ijumaa na pia itazikabili timu za Iran na Morocco katika Kundi B la Michuano hiyo mikubwa Duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: