Raisi wa TCCIA Bwana John Mayanja, akizungumza na wajumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa ambao ni wanachama wa TCCIA.

Chama cha wenye Biashara, Viwanda na Wakulima ‘TCCIA’ jana kimezindua rasmi safari ya kusherekea mafanikio makubwa waliyoyapata katika miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.

Wanachama pamoja na viongozi wa TCCIA jana walikutana kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ambao ulifanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mbalimbali yaliyotungumzwa katika mkutano huo, kulifanyika uzinduzi rasmi wa kusherekea mafanikio makubwa ya TCCIA.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group Bw. Imani Kajula ambae ni mshauri wa masuala ya masoko, Alisema ‘Huwezi kuongelea Uchumi wa nchi bila kutaja kazi kubwa iliyofanywa na TCCIA hasa katika kuleta msukumo mkubwa kwenye uboreshwaji wa sera mbalimbali ambazo zimesaidia katika kukuza Uchumi wetu. 

Miaka 30 hii ni hatua kubwa sana kwa shirika la kizalendo lililowakutanisha watu mbalimbali kutoka katika kada za Biashara, Uchumi pamoja na Kilimo na kuweza kukaa pamoja kwa maslahi mapana ya nchi yetu’

Pamoja na ufunguzi huo, mkutano huu pia kutoa fursa kwa Rais wa TCCIA Bw. John Mayanja kuweza kutoa taarifa rasmi ya kipindi cha Oktoba 2017 hadi Mei 2018. 

Akiongea katika mkutano huo aliwasihi wafanya biashara wote kuweza kutumia jukwaa hilo kuongea na serikali ili kuweza kupata majawabu ya pamoja yatakayoibua fursa zaidi za uwekezaji nchini, ‘serikali yetu ni sikivu, ni lazima sisi tuiambie tunataka nini kwa sauti yetu moja’ alisema Rais Mayanja.
Wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya Taifa pia walipata nafasi ya kusomewa Taarifa ya Mwaka 2017, taarifa ya fedha kwa kipinndi cha Jauari – Machi 2018 pamoja na kuchagua wajumbe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: