Salamu kwa watanzania na watumiaji wa Mabasi haya, pia nitumie nafasi hii kuwapa pole sana kwa adha wanayo/mnayokuwa mnaipata.

Itakumbukwa mara baadaa ya kuanzishwa kwa mabasi ya Mwendokasi abiria wengi tulisema sasa adha ya Usafiri imekwisha, lakini sasa imekuwa kinyume chake kwani;

Mabasi hayana Muda maalumu wa kuondoka na kufika katika vituo hasa vituo vikubwa mfano kivukoni terminal hii hupelekea abiria wengi kujazana wakisubiria usafiri na kupoteza maana sahihi ya MABASI YA MWENDO KASI na hata magari yakichelewa kufika hufika machache ambapo watu hujazana hadi kuzidi uwezo wa gari hivyo abiria wanabanana na kusababisha adha kubwa hasa kwa akina mama wenye watoto wadogo.

My take: SUMATRA wapewe jukumu la ku-regulate usafiri huu hasa katika kuwapangia muda.

Utoaji wa Tiketi sio rafiki.

Kwanza kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakatisha tiketi kugoma kutoa chenji ndogo zinazobakia yaani Tsh 50/= kwa kisingizio cha kuwa hawana chenji hii sio sawa na inawafanya abiria kulipia Tsh 700/= kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.

My take; Vituo vya kukatia tiketi viwe na chenji za kutosha ili kupunguza adha ya abiria kupoteza chenji zao na kwa ushauri tu kuondoa mkanganyiko huu ni vyema bei ikawa kamili yaaani Tsh 600 /=

Kwa Siku ya leo tarehe 11/06/2018 Vituo kama GEREZANI, KIVUKONI NA UBUNGO T. Tiketi haziwi SCANED Kwenye mashine na badala yake abiria ukipewa tiketi yako unapoingia mlangoni WANAICHANA NUSU kama alama. HII INAWEZA KUPELEKE WATU KUUZIWA TIKETI MARA MBILI HASA NYAKATI ZA USIKU KWANI TIKETI ISIPO CHANWA NA IKAOKOTWA INAWEZA KUUZWA TENA KITU AMBACHO KITAENDA HATA KUIBIA SERIKALI HASA KATIKA UPANDE WA KODI.

My take: Mashine za kusacan zirudishwe haraka kwa lengo la kuboresha zaidi na sio kama ilivyo kwa siku ya leo.

Mwisho; MAGARI haya yameletwa na serikali yetu sikivu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo malengo mojawapo kati ya mengi ni kupunguza adha za usafiri kutoka sehemu mbalimbali za jiji la DSM. Watumiaji tunawaomba wasimamizi wa MAGARI haya kuboresha kila siku huduma hii na sio kuangalia maslahi pekee, na naamini wasimamizi wa magari haya ni wasikivu na wamesikia kilio hiki.Asante sana!!

Adam Raphael Kihaka.
Mtumiaji na mpenda maendeleo.
0755460873
Kigamboni_DSM.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: