Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKT) Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Mch. Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Newton John Maganga, mkoani Tabora leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
---
Siku za hivi karibuni kumeibuka UTOVU WA NIDHAMU ambao unaashiria UKAIDI wa KUTOTII MAMLAKA.
Mimi ninayeiandika makala hii fupi nimekua katika malezi ya kichungaji chini ya Babu yangu ambaye ndiye mmoja wa Wachungaji walioeneza injili kwa mara ya kwanza katika Nyanda za Juu Kusini ( Iringa , Njombe ) huku akiweka makazi yake makuu pale Ilembula katika Wilaya ya Wanging’ombe . Nyakati zote kupitia maisha yake ya kila siku nilijifunza UTII na UNYENYEKEVU.
Ingekuwa ninasema na viongozi wa Serikali ningeitumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelimisha / kukumbushia juu ya UTII na UNYENYEKEVU sambamba na falsafa za Mwl. Nyerere.
Kwakuwa leo ninaandika kwa majonzi na mahsusi kwa Wanaotumika katika kuujenga mwili wa KRISTO YESU basi ungana nami huku ukiniruhusu kutumia maandiko ya Biblia Takatifu.
- Warumi 13:1 inasema “ Kila mtu na ATII MAMLAKA iliyo KUU ; kwa maana HAKUNA mamlaka ISIYOTOKA kwa MUNGU; na ile iliyopo umeamriwa na MUNGU “
Hivyo basi kutokana na Warumi 13:1 tunapata kukumbushwa KUTII MAMLAKA (SERIKALI & UONGOZI) na kwa kutokufanya hivyo unakuwa unafanya UASI wa NENO la MUNGU.
- Isaya 1:19 inasema “ MKIKUBALI na KUTII mtakula MEMA ya NCHI “
MUNGU ikiwa ameachia BARAKA juu ya Tanzania hivi leo, watakaofanikiwa KUIONA na KUNUFAIKA nayo ni wachache tu nao ni waliokubali KUTII , hivyo basi si ajabu kusema WALALAMIKAJI walio wengi hupigwa UPOFU na KUSHINDWA KULA MEMA ya Nchi.
Tito 3:1 inasema “ UWAKUMBUSHE WATU KUNYENYEKEA kwa wenye UWEZO na MAMLAKA , na KUTII na KUWA TAYARI KWA KILA KAZI NJEMA”
Siku za hivi karibuni tumemsikia MKUU WA NCHI akishauri taasisi za Dini kufanya KAZI NJEMA yenye kumzalia MUNGU matunda, ni lazima kwangu na kwa ndugu zangu viongozi wa Dini KUNYENYEKEA na KUWA TAYARI KWA KILA KAZI NJEMA.
Waebrania 13:17 inasema “ WATIINI WENYE KUWAINGOZA na KUWANYENYEKEA ; maana wao wamekesha kwa ajili ya roho zetu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa FURAHA wala Si kwa KUUGUA; maana isingewafaa ninyi “
AMANI inayochezewa na baadhi ya viongozi wa Dini ni vyema tukarejea Waebrania 13:17 na kutambua kuwa inamaanisha yafuatayo isemapo :
= Wao wanakesha : Viongozi hao ambao wanaiongoza nchi hufanya kazi kwa kutumia vyombo vilivyo chini ya mamlaka yao kukuhakikishia wewe Mchungaji AMANI ili jumapili baada ya ibada isitokee WIZI wa kuchukua SADAKA ZOTE kisha wakatokomea na hata katika nyakati za sikukuu tumejionea Askari wa Jeshi la Polisi wakilinda nyumba za Ibada huku lengo kuu likiwa ni kuimarisha AMANI.
= Watu watakaotoa hesabu : Hawa tunaotaka kuwavuruga wao ndiyo watatoa hesabu hivyo basi ndiyo maana Wama kila sababu tena wanastahili kukemea kila KENYA dalili ya kuleta uvunjifu wa AMANI utakopelekea kuleta MADHARA HASI kwa wasio na hatia.
= Maana isingewafaa ninyi : Majukumu ambayo viongozi wa Serikali wanayabeba ni majukumu mazito ambayo kwa hakika yanahitaji moyo wa kipekee wa kujitoa kama ambavyo MKUU WA NCHI anavyosema AMEJITOA SADAKA kwa ajili yetu wana wa Tanzania.
1 Petro 5:5 inasema “ Vivyo hivyo ninyi VIJANA, WATIINI WAZEE. Naam, ninyi nyote jifungeni UNYENYEKEVU, upate kuhudumiana; kwa sababu MUNGU HUWAPINGA wenye KIBURI lakini HUWAPA WANYENYEKEVU NEEMA. “
Ndugu zangu,
Hapo juu nimejaribu kuonyesha maandiko yanasema nini kabla hatuajaanza mjadala wetu. Ni vyema tukatambua kuwa MANUAL BOOK kuu ya mwana wa KRISTO si kitu kingine bali ni BIBLIA.
Hivyo basi ikiwa MANUAL BOOK au KATIBA YETU KUU ni BIBLIA kuikaidi au kwenda kinyume na maandiko ni DHAMBI na kama tunavyojua DHAMBI NI MUASI.
Usiruhusu kuwa MUASI bila ya sababu ya msingi.
MUNGU akubariki wewe unayesoma na kukusaidia katika mahitaji yako sambamba na kukulinda.
MUNGU Ibariki Tanzania
MUNGU wabariki wenye mamlaka
MUNGU wabariki wana wa Tanzania
======= AMEN ========
@ BAGATECH
Godwin D. Msigwa
Dar es Salaam
Tanzania
7 Juni 2018
Toa Maoni Yako:
0 comments: