Na Amini Mgheni - UDSM.
Ninamfahamu kwa kiasi kutokana na wajibu wangu wa kikazi licha ya kuwa alikuwa mfanyakazi wa Chuo kikuu cha Dar-es -Salaam na kwakuwa mimi nipo kwenye media za chuo nimefanya naye mahojiano ya uchambuzi wa mambo mbalimbali kama mtaalam wa sayansi ya siasa kiasi cha kutosha kumfahamu msimamo wake, utu wake,uzalendo wake kwa nchi,uadilifu wake lakini ukaribu wake na wananchi wa kawaida.
Tofauti kubwa ya kwanza baina ya Dkt. Bashiru na wasomi wengine yeye hakujifungia chuo kikuu kufundisha tu pekee,alikuwa mtu wa kutoka na kujichanganya na makundi ya jamii na kuonyesha mchango wake kama msomi pale alipoona hapa panahitajika kuchangia uelewa kwa jamii.
Dkt. Bashiru Ally (mkulima) nilimuona kwenye baraza la wakulima, alikuwa ni miongoni mwa wasomi waliochangia kwa kiasi kikubwa katika baraza la wakulima kwa kuwaelekeza kufanya kazi kwa badiii na kuwa na mfumo wa kilimo chenye tija kwa wananchi wa kawaida.
Dkt. Bashiru Ally (Haki za ardhi) nilikuwa pia namuona ama kukutana na Dr Bashiru Ally kwenye harakati za shirika la Haki Ardhi lililokuwa na wajibu wa kusaidiana na serikali na jamii kuelemisha wananchi juuu ya umuhimu wa ardhi lakini matumizi sahihi ya ardhi na kwa upekee wakati huo hatua za uwekezaji wa mazao ya nishati mabadala yalivyokuwa yanatishia kupoka ardhi ya vijjiini nzuri kwa kilimo alipaza sauti sana kupiga hilo kwa hoja.
Dkt. Bashiru Ally (mswahili na mshairi) mara kwa mara katika mijadala ya sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha daresalam wakati wasomi wengine wakiandaa mada yeye alikuwa anaandaa ushaairi na kusoma ushairi ule kufikisha hoja yake,DR Bashiru ni mswahili mzuri sana.
Dkt. Bashiru Ally (mmajimui wa Afrika) moja ya hoja ya kipekee ambayo ukikaa naye kidogo tu utagundua namna ambavo amekuwa akiendeleza hoja za uafrika na namna ambavyo bado anaamini katika waafrika kujiendeleza wao wenyewe na kutimia talanta zao na rasilimali kujikuza kiuchumi.
Dkt. Bashiru Ally (Muumini mkubwa wa Azimio la Arusha) nimemuona mara kadhaa katika mijadala mbalimbali kisisitiza na kuamini kuwa Azimio la Arusha bado ni nyaraka muhimu ya kipekee ambayo kama taifa tunapaswa kuirejea na kufanyia kazi kwani imejaa utu na uzelendo kwa taifa.
Dkt. Bashiru Ally (Msawa wa kijinsia) ndio nimewahi pia kumkuta kule TGNP akiwaeleza wananchi wanyonge juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia na akiwaelezea namna ambavyo kila mtu anapaswa kusimama na kujali makundi ambayo hayapewi nafasi kwa sababu mbalimbali alijishusha na kukaa nao chini na kuwapa elimu.
Dkt. Bashiru Ally (mnyenyekevu asiye penda atambulishwe kama msomi) ndio mara nyingi hakupenda kuitwa Daktari wa falsafa na mpaka leo ukimhoji bado atakuambia naitwa Bashiru Ally ni mtu ambaye hakuubeba usomi kwa kujivuna, aliubeba usomi kama utumishi kwa watu wengine na taifa lake tofauti na wengi wenye nafasi na usomi wa kabila yake.
Haya ni machache sana ninayomfahamu nayo,najua wapo wanaomfahamu zaidi ya mimi,kazi moja ya msingi ambayo anayo ni kukiweka chama kwenye dhama zingine kabisa ambapo uzalendo, utu, kujitolea kwa wana-CCM kujenga taifa lao na kujenga chama chao sasa kutakuwa ni kwa zaidi.
Ana kazi kubwa ya kukitoa chama kwenye falsafa ya watu kwenda kuchota fedha na kukipeleka kwenye dhana ya watu kuombwa kujitolea kulitumikia taifa lao kupitia chama.
Ana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa sasa katika uchaguzi mkuu ujao CCM itaeleweka zaidi na wagombea wake watakuwa na kazi rahisi ya kujielezea na kuweka wazi yapi wamefanya.
Ana kazi ya kuhakikisha kuwa sasa wanapatikana wagombea makini wa ubunge na udiwani ambao kweli watabeba falsafa ya chama, na kuhakikisha kuwa wagombea ubunge wa chama sasa wanakuwa watu wenye uelewa mkubwa zaidi na kuweza kukabiliana na wapinzani kwa hoja za maana na kurahisisha wa Rais kuteua mawaziri kutoka katika kundi la wabunge bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments: