Wakulima wa zao la korosho wilaya ya Tandahimba na Newala mkoani Mtwara wamelalamikia kitendo cha kampuni ya JOPHULO LIMITED kutowalipa fedha zao zenye thamani zaidi ya Shilingi bilioni 3 tangu kufanyika kwa mnada wa 11 Disemba mwaka jana .
Wakizungumza na Ruvuma Tv , wakulima hao wanasema hali hiyo inawafanya kushindwa kujipanga na msimu mpya wa kilimo ambapo wanatumia nafasi hii kuomba serikali kuingilia kati sakata hilo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: