Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Milama, iliyopo mkoani Morogoro baada ya kukabidhi mbegu bora ya mahindi ya Wema 2109 kwa ajili ya shamba darasa. Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani humo leo.


Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli  (katikati) mbegu ya Wema 2109 kwa ajili ya kuwakabidhi wakulima wa wilaya yake ili waanzishe mashamba darasa. Wengine kutoka kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mvomero, Hilali Focus Riddy, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mvomero, Daina Muywanga na kulia ni Mtifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu.

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi, Mvomero wakiandaa shamba kwa ajili ya kupanda mbegu ya Wema katika shamba darasa.
 Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel (kushoto), akizungumza katika uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi Mvomero.
 Uzinduzi ukiendelea.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi Mvomero.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakikabidhiwa mbegu hiyo ya Wema.
 Mkulima Yacob Patrick, akikabidhiwa mbegu hiyo.
 Mkulima Mohamed Maungo, akikabidhiwa mbegu.
 Mkulima Tatu Mbonde, akikabidhiwa mbegu.
 Walimu wa Shule ya Msingi Mvomero wakikabidhiwa mbegu.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mvomero.

 Mtifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu ambao ndio waliofanya utafiti wa mbegu hiyo, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu hiyo.

 Uzinduzi wa shamba darasa katika shule ya msingi Mvomero.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mvomero wakiwa katika upandaji wa mbegu hizo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utalli akizindua shamba darasa kwa kupanda mbegu hiyo ya Wema 2109.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utalli, akizungumza na wakulima wanaounda kikundi cha Tupendane kilichopo Kijiji cha Didamba.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Kijiji cha Didamba,  Mwanahamisi Omari (kushoto), akikabidhiwa mbegu.
 Mkulima  Maulid Adamu kutoka Kikundi cha Kazibanza kilichopo Kijiji cha Milama akikabidhiwa mbegu.

Na Dotto Mwaibale, Mvomero-Morogoro.

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi ya Mvomero mkoani Morogoro wametakiwa kujikita zaidi katika masomo ya Sayansi ili waweze kulisaidia taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti.

Mwito huo umetolewa wilayani humo leo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabani Hussein wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi ya Wema E2109 inayostahimili ukame iliyotolewa na COSTECH kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

"Ninyi wanafunzi nawaomba someni sana masomo ya sayansi ili hapo baadae muweze kuwa watafiti wa masuala mbalimbali jambo litakalosaidia taifa" alisema Hussein.

Alisema tafiti zozote zinafanywa na wataalamu waliobobea katika masomo sayansi hivyo aliwataka wanafunzi hao kujifunza kwa bidii masomo hayo ya sayansi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo, Mohamed Utalli aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kupeleka mradi huo katika wilaya yake ambapo amewataka wananchi kuzichangamkia mbegu hizo.

"Tuna bahati sana katika mkoa wetu kwani katika mikoa tisa ambayo mradi huo utafanyika na sisi tupo hivyo ni fursa kwetu tusiiache ikapotea bure" alisema Utalli.

Utalli aliwataka wakulima wilayani humo ulimopita mradira huo kuhakikisha wanayatunza mashamba hayo ili kuleta tija katika zao la mahindi.

Alisema mradi huo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kufanya kazi kwa bidii wakati taifa likiingia katika uchumi wa kati wa viwanda.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel  alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu  Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni wakulima.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.

Mtifiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.

Aliongeza kuwa mbegu hiyo italeta matokeo mazuri iwapo kanuni za kilimo bora zitafuatwa kama vile kufuata vipimo, maandalizi ya shamba, matumizi ya mbolea zote ya kupandia na kukuzia na kuwa mbegu hiyo ni moja kati ya mbegu 11 zilizofanyiwa utafiti.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: