Kumekuwepo na taarifa inayosambaa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amewafukuza kwenye ofisi zake wabunge Halima Mdee (Kawe) na Saidi Kubenea (Ubungo). Baada ya kufanya mawasiliano na DC Hapi ukweli ni huu ufuatao:-

1. Uamuzi wa kuwaondoa wabunge hao ulifanyika katikati ya mwaka jana 2017.

2. Si Halima Mdee na Kubenea pekee walioondolewa. Bali Mdee (Kawe), Mnyika (Kibamba) na Kubenea (Ubungo) wote waliandikiwa barua kuwataka wahame wakipewa notisi ya kujiandaa.

3. Wabunge wote hao walikua hawana ofisi majimboni kwao walikochaguliwa (Kawe, Kibamba& Ubungo)na badala yake ofisi zao zilikua kwenye Jimbo la Kinondoni kwa Mkuu wa wilaya.

4. Uamuzi wa kuwaondoa ulilenga kuwafanya wakatafute ofisi kwenye majimbo yao kwa wananchi waluowachagua mwaka 2015 ili kuimarisha demokrasia.

5. Wabunge wote hao watatu hawakua hata na ofisi za kupanga kwenye majimbo yao hivyo kuwafanya wananchi kupata taabu ya kuwafikia.

6. Hakuna Sheria inayomtaka Mkuu wa wilaya kuwapa ofisi wabunge hao isipokua utashi. Wabunge wengine wana ofisi zao Binafsi.

7. Ofisi walizoondolewa Halima Mdee, Kubenea na Mnyika zilihitajika kwa matumizi mengine ya serikali chini ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi.

8. Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni iko katika Jimbo la Kinondoni.

Huo ndio ukweli wa wabunge hao kuondolewa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: