Balozi wa China nchini Bi. Wang Ke (kulia) kwa kushirikina na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakizindua ujenzi wa ofisi za walimu katika shule ya Sekondari Makumbusho. 

Na Mwandishi Wetu.

Ubalozi wa China Nchini Tanzania umeguswa na kazi nzuri inayofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuboresha mazingira ya walimu na kuamua kumzawadia Majengo Matano ya kisasa kwaajili ya ofisi za walimu ambapo leo RC Makonda ameweka jiwe la Msingi kuashiria kuanza kwa Ujenzi huo kwenye Shule ya Sekondari Makumbusho pamoja na kukabidhi Ramani ya jengo.

Ujenzi wa Majengo hayo Matano ni matokeo ya RC Makonda kuwasilisha ombi la ujenzi wa ofisi za walimu kwa Balozi wa China nchini Tanzania na kwakuwa kazi anayofanya RC Makonda inaonekana Balozi huyo alipokea kwa mikono miwili ombi hilo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia katika uzinduzi wa ujenzi wa majengo ya ofisi za waalimu katika shule ya Secondari Makumbusho ulifanyika leo ambapo Balozi wa china amezindua na kuaahidi kujenga majengo hayo kwa wilaya zote za mkoa huo.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Makumbusho wakiwa na utulivu.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Yatajengwa kwenye Wilaya Tano za Mkoa wa Dar es salaam ambapo ndani yake zitakuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi, Ofisi ya walimu wote, ukumbi wa mikutano, chumba cha kuhifadhi mitihani, vifaa vya michezo, chumba cha muhasibu, chumba cha kubadili nguo, mapokezi, vyoo, bafu huku zikisheheni furniture za kutosha ikiwemo viti, meza, makabati na AC ambapo ujenzi wa jengo hilo unataraji kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.

RC Makonda amemshukuru Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke kwa ujenzi wa majengo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaenda kupunguza mateso ya walimu kufanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kufanya kazi kwenye madarasa.

Amesema dhamira yake kuboresha mazingira ya walimu ni kuwawezesha kutoa elimu bora itakayowezesha Taifa kuwa na wataalamu wa kutosha.

Kwa upande wake Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke amesema kwa miezi mitatu aliyoishi hapa nchini tangu alipoteuliwa kuwa balozi ameshuhudia maendeleo makubwa aliyofanya RC Makonda hivyo wameona wasikae kimya kwenye jambo hilo linalolenga kuleta ukombozi wa uchumi kupitia elimu.

Nao walimu wa shule ya makumbusho wamemueleza RC Makonda kuwa awali walikuwa wakitumia madarasa manne ya wanafunzi hivyo ujenzi wa jengo hilo ni neema kwao kwakuwa madarasa hayo yatarejeshwa kwa wanafunzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: