Mkurugenzi Mtendaji wa Imetosha, Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Kansa Duniani ambayo Taasisi ya Imetosha imeratibu upimaji wa watoto leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watu wenye ualbino wakiandisha kwa ajili ya upimaji katika Hospitali ya Ocean Road leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watu wenye ualbino wakiwa wamekaa kwa ajili ya kwenda kupata taraibu za upimaji katika Ocean Road leo jijini Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii).
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Imetosha, Henry Mdimu amesema kuwa watoto wenye ualbino kati watano hadi saba wanafariki kwa mwezi katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na Kansa ya ngozi.
Mdimu ameyasema hayo wakati wa upimaji wa kansa kwa watoto wenye ualbino katika Hospitali ya 0cean Road katika Maadhimisho ya Siku ya Kansa Duniani ambayo huadhimishwa Februari 3 kila mwaka.
Amesema kambi ya upimaji huo wameshirikiana na Hospitali ya Ocean Road na Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS) katika kuhakikisha kila mtoto mwenye ualbino anapata vipimo.
Amesema kambi ya upimaji hiyo itaendelea mikoani ambayo watapima madaktari wa Ocean Road ili kujua hali ya tatizo ya Kansa kwa watoto wenye Ualbino na baada ya kupimwa na kuonekana kuanza kupatiwa matibabu.
“Mimi Mkurugenzi wa Imetosha naona nina wajibu wa kuwa moja kwa moja na watu wenye ualbino kuhakikisha maisha ya watoto yanaokolewa nikifanya mimi na mwingine atafanya”amesema Mdimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: