Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akifungua kongamano la huduma jumuishi za kifedha wenye lengo la kukuza upatikanaji wa huduma hizo kupitia mifumo ya teknolojia za kidijitali kati ya benki ya FINCA na MasterCard Foundation lililofanyika jijini Dar Es Salaam leo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya FINCA Tanzania, Issa Ngwegwe akizungumza kwenye Kongamano la huduma jumuishi za kifedha wenye lengo la kukuza upatikanaji wa huduma hizo leo jijini Dare Es Salaam.
Wadau wakifuatilia jambo.
Mkurugenzi Mtendaji FINCA Canada, Ms.Stephanie Emond akizungumza kwenye kongamano
Mkurugenzi Uendeshaji wa FSDT Irene Majede akielezea jambo kwenye kongamano la Huduma Jumuishi za Kifedha leo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (katikati)na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Yamungu Kayandabila wakiwa na picha walizokabidhiwa kutoka kwa Afisa Mtendaji mkuu wa Benki ya FINCA Tanzania, Issa Ngwegwe(wapili kulia). Wengine kulia ni Mkurugenzi Mtendaji FINCA Canada, Stephanie Emond na mwisho kushoto ni Mkurugenzi Uendeshaji wa FSDT, Irene Majede Mlola, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Kongamano la huduma jumuishi za kifedha wenye lengo la kukuza upatikanaji wa huduma hizo leo jijini Dare Es Salaam
Wadau wakifuatilia jambo.

Benki ya kutoa mikopo midogo midogo inayoongoza Tanzania FINCA Micro-Finance Bank, kwa kushirikiana na MasterCard Foundation, taasisi ya kimataifa ambayo inatoa ushirikishaji wa kifedha na kuendeleza elimu kwa vijana barani Africa, leo imefanya mkutano wa siku moja wa Ushirikishaji wa Kifedha jijini Dar es Salaam wenye lengo la kushirikishana ujuzi miongoni mwa wadau mbalimbali katika kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia katika mifumo mbalimbali ya kidigitali.

Mkutano huo, ulilenga kutathmini mafunzo yaliyotolewa kwa miaka mitano ya ushirika baina ya FINCA na Mastercard Foundation kwa lengo la kukuza huduma za kifedha kwa jamii ya watu walio katika sekta isiyo rasmi katika nchi za Tanzania, Zambia na Malawi kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na watoa huduna za kifedha, wafadhili, watafiti na wasimamizi wa sekta za kifedha, kubadilishana mawazo kwa lengo la kukuza upatikanaji na matumizi za huduma za kifedha Tanzania.

Katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa FINCA, Tanzania, Issa Ngwegwe alisema “mifumo ya teknolojia ya kidigitali ni kichocheo kikubwa sana katika ushirikishaji wa kifedha na pia maendeleo ya mfumo wa kidigitali ni muhimu katika kuongeza upatikanaji wa huduma hizo.”

"Mifumo ya kidigitali ya simu za mkononi na wakala wa kibenki ni vipengele muhimu katika kupunguza bei ya kuwafikia mamilioni ya watanzania ambao hawana huduma za kibenki. Ushiriki na mitandao ya simu inaonyesha fursa ya kukuza upatikanaji wa huduma za kifedha. “ Aliongeza.

Akiongea katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendji wa wa FINCA Canada Bi. Stephanie Emond alisema kwamba ushiriki wa Mastercard Foundation umeweka misingi mizuri ya ukuwaji kwa kupitia matumizi ya teknolojia ya kifedha na mafunzo kwa lengo la kuboresha huduma na kukuza uwezo wa FINCA pamoja na uelewa mzuri zaidi wa mahitaji ya wateja na matokeo ya mipango ya ushirikishwaji wa fedha kwao.

“Tunaamini kwamba kupitia mkutano huu tutajifunza kutoka safari yetu na tujenge uhusiano wa karibu miongoni mwetu pamoja na nafasi nzuri ya kukabiliana na changamoto za soko alikadhalika na kuweka mazingira mazuri kwa ukuwaji wa huduma za kifedha na uendeshwaji wa sekta hiyo.” Alisema Bi. Stephanie.

Kwa upande wa mgeni rasmi Dr. Ashatu Kijaji, Naibu waziri wa fedha na Mipango alisisitiza kuwa serikali imekusudia kukuza ushirikishaji wa kifedha kupitia uwekaji wa kanuni stamilifu na uratibu mzuri pamoja na mazingira mazuri kwaajili ya ushirikishaji wa kifedha ambao utapeleka huduma za kifedha kwa watu maskini kukiwa na hatua stahiki za kumlinda mtumiaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: