Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimmkabidhi nyenzo za kazi Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Mhe. Dotto Mashaka Biteko akiongea machache baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Spika Job Ndugai akizungumza machache baada ya Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini waliohudhuria kwenye hafla ya kuapishwa Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.

Na Mwandishi Wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanika madudu ya Wizara ya Madini akisema kuwa baadhi ya wateule wake katika wizara hiyo wamekuwa wazembe katika kutekeleza maagizo na kutimiza majukumu yao kama watendaji wa serikali.

Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais ametolea mfano wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa bungeni mwezi Julai mwaka jana, ambapo amesema mpaka sasa wizara hiyo haijapitisha kanuni (regulations) ili sheria hiyo iweze kufanya kazi jambo ambalo amesema ni uzembe usiovumilika huku akimwagiza Waziri wa Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kukamilisha kanuni hizo na kuzisaini kufikia Ijumaa ya wiki hii.

“Nakushukuru Mhe spika kwa kutoa ushauri kwa serikali na sisi tumekuwa tukiufuata sana. Wizara ya madini ina changamoto sana na hata sasa ina changamoto na haifanyi kazi vizuri. Spika utakumbuka mwezi wa saba mlifanya marekebisho ya sheria ya madini. Na ilipokuja kwa kwangu siku hiyo hiyo nilisaini na kuipitisha, lakini tangu Julai mpaka sasa regulations (kanuni) hazijasainiwa lakini sheria imepitishwa na bunge, hivyo sisi Watanzania watumishi hatupo serious.

“Nasikitika kusema baadhi ya ninaowateua hawajajua nataka nini. Ndiyo maana nikamteua aliyekuwa kwenye kamati ya madini, labda atatoa changamoto kwa wenzake maana huenda yeye anaelewa zaidi. Na mnada wa Tanzanite hautafanyika tena mpaka regulations zitakaposainiwa. Sasa mpo manaibu wawili na waziri wa sheria yupo hapa nataka regulations hizi zisainiwe kabla ya Ijumaa, tumeibiwa mno, sasa nimesema imetosha,” alisema Rais Magufuli kwa uchungu
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: