Katibu Tawala wilaya ya Temeke, Hashim Komba akikabdhi mfano wa hundi kwa mshindi wa mchezo wa bahati nasibu wa Tatumzuka Enirisha Kilango mapema leo kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke. Enirisha Kilango ambaye ni Mkazi wa Temeke Mikoroshini anaejishughulisha na biashara zake ndogo ndogo alijishindia milioni 50 mwishoni mwa wiki.
Katibu Tawala wilaya ya Temeke, Hashim Komba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Temeke, mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo, kabla ya kukabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa mchezo wa bahati nasibu wa Tatumzuka kwa mshinidi aliyejinyakulia Enirisha Kilango aliyejishindia milioni 50 mwishoni mwa wiki.
Komba amewashukuru Tatumzuka kwa kuendelea kuwawezesha wananchi wa wilaya hiyo ya Temeke kupitia mchezo huo wa bahati nasibu, kwa kumpata mshindi mwingine ndani ya wilaya hiyo kwa mara nyingine tena,Komba amewasisitizia wananchi wake kuendelea kucheza zaidi na zaidi kwani mchezo ambao upo kisheria na hauna makando kando yoyote,ukishinda umeshinda kweli na fedha zako unakabidhiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: