
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Longido(wa pili kulia) wakimsikiliza Mhandisi wa Maji wilayani Longido,Ramadhani Musiba(kushoto) utekelezaji wa miradi ya maji.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda(kushoto) akipanda ngazi kukagua mradi wa maji wilayani Longido,akiwa na Mkuu wa wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,Godfrey Chongolo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda akipanda ngazi kukagua mradi wa maji kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa wilayani Longido.
Ujumbe wa Naibu Waziri wa Tamisemi,Joseph Kakunda pamoja na maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Longodo wakikagua moja ya miradi ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.
Mhe. Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakijumuika na wananchi kuimba wimbo wa kufurahia mradi wa maji.
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakiagana na wananchi wa Kijiji cha Ranchi.
Na Mwandishi Wetu, Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda amepongeza ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa katika mpango wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya
Tabia Nchi katika wilaya za Longido,Monduli na Ngorongoro.
Mradi huo unaosimamiwa kwa pamoja na Ofisi ya Rais-Tamisemi,taasisi ya kimataifa ya maendeleo na mazingira(IIED) na Haki Kazi Catalyst unatarajiwa kuwanufaisha wananchi walio katika wilaya hizo tatu.
Akiwa katika Kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa alipongeza hatua iliyofikiwa ya kuwawezesha wananchi kupata maji safi kwaajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na mifugo yao ikizingatiwa wilaya ya Longido asilimia 95 ya wakazi wake ni wafugaji.
Amesema mkandarasi amekua mzalendo kwa kujenga miundombinu ya maji tenki pamoja eneo la kunyweshea mifugo kwa thamani ya Sh 36 milioni na kuonya nwakandarasi wasio na uzalendo wanatekeleza miradi kwa gharama kubwa lakini inakua haina ufanisi.
Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo amesema wilaya yake ipo jumla ya miradi 14 inayofadhiliwa na IIED kwa lengo la kuwawezesha wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.







Toa Maoni Yako:
0 comments: