Wanaharakati wa kata ya Kipunguni wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana jijini Dar es salaam.
Mchungaji wa kanisa la Sinai Pentecostal Ndugu. Imani Juma Feruzi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika pikipiki mapema jana, katika uzinduzi wa kampeni ya akeketwi mtu mwaka 2018 iliyoandaliwa na Sauti Jamii Kipunguni ili kupinga vitendo vya Ukeketaji na Rushwa ya ngono. 
Mwanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni Bi. Tausi Msangi akibandika karatasi yenye ujumbe(posters) katika moja ya duka la dawa linalopatikana katika kata ya kipunguni, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.
Wanaharakati wa Sauti Jamii Kipunguni wakiwa na watoto mbalimbali wa kata ya hiyo wakiwa wameshika mabango yenye jumbe tofauti tofauti kuashiria kuchoshwa na vitendo vya ukeketaji vilivyoshamili katika kata hiyo, mapema jana katika uzinduzi wa kampeni ya Akeketwi mtu mwaka 2018.

Na Vicent Macha

Kituo cha sauti jamii Kipunguni jana tarehe 29 mwezi desemba kimezindua kampeni mahususi ya kutoa elimu mtaa kwa mtaa, iliyofuatiwa na zoezi kugawa vipeperushi pamoja na kubandika karatasi zenye jumbe mbalimbali katika kata hiyo.

Akiongoza kampeni hiyo Mkurugenzi wa Sauti jamii Kipunguni Bw. Selemani Bishagazi alisema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo kuangazia sehemu kuu mbili ambazo ni kupinga ukeketaji katika kata hiyo lakini pia rushwa ya ngono katika jamii ya kitanzania.

Aidha Bw. Bishagazi alidai kuwa kampeni hiyo imelenga kupinga vitendo vya ukeketaji ambavyo vinavyotarajiwa kutekelezwa mwakani 2018 kwani ndio mwaka mahususi kwa kukeketa hususani kwa makabila yanayotokea mkoani mara ambayo yameshamili katika kata hiyo.

Aliendelea kusema kuwa watekelezaji wakuu wa mambo haya ni watu tunaoishi nao katika jamii zetu na kesi zake zinakuwa ngumu kusikilizwa kutokana kwamba watekelezaji wa hayo ni baba, mama au shangazi hivyo inaleta ugumu katika kutoa ushahidi na mtoto anaogopa kwa kuwa anajua mzazi wake au ndugu yake atafungwa kwa sababu yake.

“Wanaharakati wengi wamekuwa wakisubiri zoezi la kukeketa lianze ndipo waanze kuwakamata wahusika wakiwa tayari wameshakeketa, lakini kwetu sisi tumeona tuzuie kabla watoto hawa hawajafanyiwa ukeketaji ili kuweza kuwakomboa juu ya mila na tamaduni mbaya kama hizi” alisema bishagazi .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: