SIKU MOJA NABII SULEIMAN (A. S) ALIKUWA AMEKAA UFUKWENI MWA BAHARI.
Mara akamuona sisimizi akiwa amebeba punje ya nafaka akielekea ktk bahari.
Nabii suleiman ikawa anamtazama yule sisimizi anapoelekea mpaka akayakaribia maji mara akamuona chura, Akiwa amekitoa kichwa chake nchi kavu haliyakuwa ameufumbua mdomo wake, yule sisimizi akaingia katika mdomo wa yule chura.
Kisha yule chura akazama ndani ya maji yakapita masaa mengi nabii Suleiman A.S akitafakari jambo lile la ajabu.
Mara akatoka yule chura ndani ya maji akaufumbua mdomo wake na akatoka yule sisimizi ilihali akiwa hana tena ile punje ya nafaka.
Nabii Suleiman A.S akamuita yule sisimizi na kumuuliza kilichoendelea na alikuwa wapi?
Yule sisimizi akamjibu "ewe mtume wa Mwenyezi Mungu hakika katika kina cha bahari hii unayoiona, kuna mawe makubwa.
Katika mawe hayo kuna mashimo ndani ya mashimo hayo kuna mdudu haoni (kipofu)
Mwenyezi Mungu amemuumba huko huyo mdudu, hawezi kutoka na kutafuta riziki, Mwenyezi mungu amenichagua mimi kumfikishia yule mdudu rizki yake,
Chura huyu hunihifadhi mimi katika mdomo wake ili nisidhuliwe na maji akinifikisha katika mashimo ya yale mawe hufumbua mdomo wake, Kisha mimi huingia ndani ya mashimo yale na kumpa yule mdudu punje ile ya nafaka kisha nikitoka chura hunirudisha tena nchi kavu."
Nabii Suleiman A.S akamuuliza yule sisimizi "je unamsikia huyo mdudu akisema chochote?"
Sisimizi akajibu "ndiyo mdudu yule husema, !ewe mwenyezi Mungu ambae hujanisahau mimi (kwa kunipa riziki yangu) nikiwa katika kina cha bahari, Ewe mola usiwasahau waja wako waumini kwa huruma yako."
mwisho
Ewe ndugu yangu ikiwa mwenyezi Mungu hakumsahau mdudu ambae haoni tena aliye katika kiza cha bahari. Vipi akusahau wewe mwanadamu?
Ni juu yetu wanadamu kutokata tamaa juu ya riziki kwani tambua hakuna yeyote anayeweza kuichukua au kukucheleweshea riziki aliyokupangia ALLAH.
Shukran Kwa Elimu na Allah s,w akujaalie
ReplyDelete