Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule (wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) waliohudhuria semina iliyofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Na Kajunason/MMG.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amewataka wasimamizi wa mpango wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma (PETS) kuwa na uadilifu katika kufiatilia matumizi ya fedha za serikali.

Hayo ameyazungumza leo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo uliowakutanisha viongozi wa serikali, dini na wasimamizi wa mpango wa "Public Expenditure Tracking System" (PETS) uliofanyika Same kwa kuwezeshwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Mhe. Senyamule alisema ni vyema watendaji hao wakafuata misingi imara itakayowezesha serikali kujua ni wapi wanamatumizi mabovu ya fedha katika halmashauli.

Aliagiza halmashauri kushirikiana kwa karibu na watu hao kwani kazi wanayoifanya ni ya halmashauri, hasa ukaguzi na mipango. "Idara ya ukaguzi ina watumishi 3 tu wanaohitaji kukagua kila kitu, sio rahisi wakidhi kwa wakati; lazima tuwashirikishe wadau wa PETS ili taarifa zao ziwe ni moja ya misingi ya ufuatiliaji kwa halmashauri," alisema Mhe. Senyamule.

Pamoja na yote Mhe. Senyamule aliomba CCT kuongeza idadi ya kata wanazofanyia kazi kutoka 11 hadi zote 34 zilizopo kwa sasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: