Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mhe Samia Suluhu Hassan amekwenda kumjulia hali Mhe. Lissu baada ya kutoka katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa awamu ya pili, sherehe zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhulia sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Home
HABARI MAKAMU WA RAIS
HABARI NA MATUKIO
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AMJULIA HALI MHE. LISSU JIJINI NAIROBI, KENYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments: