---
KAMPUNI ya bia nchini ya TBL imepewa tuzo ya kwanza ya matumizi bora ya magari makubwa ya mizigo ya Mercedes Benz Actros ambayo yametimiza zaidi ya kilomita milioni moja huku yakiwa bado katika hali bora.
TBL ina magari kumi ya aina hiyo ambayo yamefanya kazi kwa miaka 17.
Tuzo hiyo imetolewa na DAIMLER kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya CFAO nchini Tanzania ambayo ndiyo mawakala pekee wa magari ya Mercedes Benz nchini Tanzania.
Tuzo hiyo Mercedes-Benz Actros yenye kubeba jina la ‘Mileage Millionaire’ kutokana na kupita kilomita milioni moja, imetolewa kuonesha kuridhishwa kwa watengenezaji wa magari hayo juu ya uimara wake. TBL ina magari zaidi ya 80 ya Mercedes Benz.
Magari yote hayo yamefikisha kilomita milioni 11 katika miaka 17 ya kuwa barabarani. Kilomita hizo ni sawa na kuzunguka dunia mara 275.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo alisema katika utoaji tuzo huo kwamba wanafurahi sana kusherehekea kilomita zaidi ya milioni moja ya magari ya ACTROS.
Alisema ni mafanikio makubwa kuwa na magari hayo na hiyo inamaananisha kwamba ni imara na yanayoaminika yakiwa yametengenezwa kuhimili hali mbaya zaidi na kwamba wateja wanaweza wakawategemea kwa huduma bora za mauzo na pia uhudumiaji wa gari lenyewe ili liweze kudumu zaidi.
Akipokea tuzo hiyo mwakilishi wa Tanzania Breweries Limited, ambaye ni meneja wa lojistiki wa Afrika Mashariki James Nyoike alisema kwamba amefurahi sana kuwa sehemu ya simulizi lenye mafanikio katika uendeshaji wa kampuni kwa kuwa na magari yenye sifa kubwa wa uimara.
Alisema anafurahia huduma ya matengenezo inayopata magari yake kila yanapotakiwa kutengenezwa, pamoja na mafunzo kwa madereva hali iliyowezesha kuwapo kwa udumu zaidi kwa magari.
“Tuna zaidi ya magari 80 ya Mercedes Benz kuanzia modeli za 2000 hadi 2016. Magari haya yamethibitisha ubora wake kazini na kuwa sehemu muhimu sana ya kazi zetu hasa za usambazaji wa bidhaa” alisema Nyoike.
Katika mahojiano alisema kwamba gari lililopitisha kilomita milioni 1.5 T 418 AAT limeendeshwa na dereva mmoja Moses Ulenga kwa miaka 10.
Naye Tharaia Ahmed Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko amesema kwamba wamemua kutoa tuzo hiyo kwa TBL kama sehemu ya kuonesha namna gani ushirikiano kuanzia mauzo hadi matunzo unavyoweza kumnufaisha mtu ambaye ananunua magari hayo kutoka CFAO.
Alisema TBL imeonesha ubora wa magari hayo na kuaminika kwake katika safari ambazo wakati mwingine ni ngumu sana kwa kuzingatia mazingira vyetu.
CFAO Motors Tanzania ambayo zamani ilijulikana kama DT Dobie ni kampuni tanzu ya kundi la makampuni ya CFAO ya Ufaransa. CFAO Motors iliundwa 1952na ni wakala wa magari mbalimbali Mercedes-Benz ya kibiashara, ya abiria na ya binafsi.


Toa Maoni Yako:
0 comments: