Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa ameshika bidhaa za kampuni ya Ivori Iringa ambazo ni chocolate na pipi za maziwa alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa bi Amina Masenza walipotembelea banda la kampuni ya Ivori Iringa katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiomuonyesha waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe baadhi ya bidhaa za kampuni ya Ivori Iringa katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amezipongeza bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya Ivori Iringa (I.F.B) iliyopo mkoani Iringa.

Akizungumza wakati wa kufungua maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini katika viwanja vya kichangani mkoani Irirnga Prof. Maghembe amekuwa akitumia bidhaa za Ivori mara kwa mara bado anazipenda kutokana na ubora wake.

“Hata akija mtu kutoka nje ya nchi hawezi amini kama bidhaa kama hizi za Ivori zinatengezwa Iringa Tanzania maana zimekuwa na ubora unastahili ndio maana leo kwenye maonyesho haya nimetembelea kwenye banda hili na kukuta bidhaa mchanganyiko wa kampuni ya Ivori Iringa (I.F.B)”alisema Prof. maghembe

Aidha Prof. maghembe aliwaomba viongozi wa mkoa wa Iringa na watanzania kwa ujumla kuendelea kuzitumia bidhaa hizo kwa kuzimia kwa lengo loa kuinua uchumi wa wazalendo hasa hivi viwanda wa wananchi wazawa tuvikumbatie ili kuendelea kutoa ajira kwa wananchi wengine.

“Nimeonja hizi chocolate za kampuni ya Ivori Iringa kwa kweli kama zile ambazo huwa nazinunua nikiwa ulaya au marekani jamani watanzania wenzangu tuendelee kutumia bidhaa bora zinazotengenezwa na kampuni zetu za kizalendo” alisema prof. maghembe.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa kampuni ya Ivori Iringa imekuwa ikizalisha bidhaa bora na zenye viwango vya kimataifa ndio maana zimekuwa zikipendwa na watu wengi.

“Ukitembea karibia maeneo yote hapa nchi Tanzania huwezi kuzikosa bidhaa za Ivori Iringa kutokana na ubora wake hivyo wanasii tu waongeze wigo wa soko la bidhaa zao bila woga maana zinaubora unaotakiwa” alisema Masenza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: