Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumta Mshama. Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumtha Mshama akiwa anaonyeshwa mpaka ya eneo la kiwanja cha Kanisa la GRC Kambi ya Warbrania Mlandizi aliyepo nae ni Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Mercy Adam Mwakimomyile.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe.Assumta Mshama akiwa anaongoza maombi mara baada kuona eneo ambalo linatarajiwa kujengwa kanisa.
Mhe.Assumtha Mshama akihubiri neno la Mungu katika kanisa hilo la GRC lililopo Mlandizi.
Wa kwanza kulia ni Mchungaji Kiongozi wa RGC Kambi ya Waebrania Mercy Adam Mwakimomyile, Mama Mtume Deo Rwetaka wa Kwanza kushoto, Mama Askofu Amon Lukama wa RGC Tanzania na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumtha Mshana.
Baadhi ya waumini walioshiriki katika ibada hiyo ya Kongamano la Wanawake RGC Mlandizi.
Baadhi ya watoto wanaolelewa kanisani hapo wakiimba wimbo maalumu wa kuliombea Taifa la Tanzania pamoja na Rais wa nchi.
Ibada ya ikiendelra katika kanisa hilo la GRC Kibaha Mlandizi.
Na.Vero Ignatus, Mlandizi.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumtha mshana amewataka wanawake kutokudharau kazi hata kama ni ndogo kwani kwenye hiyo ndogo ndipo nyingine kubwa itafuata.
Ameyasema hayo Katika Kanisa la RGC lililopo Mlandizi ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la wanawake lililoambatana na Changizo kwa ajili ya kununua eneo la kiwanja cha kujenga kanisa.
Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mchungaji alipata nafasi ya kuhubiri katika kongamano hilo ambapo amewataka wanawake kujiamini na kuaajibika kwani hata neno la Mungu linasema asiyefanya kazi na asili.
"Nyumba ambayo mwanamke ni legelege nyumba hiyo haitaendelea kamwe,wanawake changamkeni wajibikeni nyie ndiyo nguzo ya familia hutamchosha mume wako" alisema
Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi Kambi ya Waebrania Mlandizi Mercy Adam Mwakimomyile amesema kuwa Kongamano hilo limebeba kaulibiu isemayo Nguvu ndani ya Mwanamke(Power in Woman) ambapo imewafanya wanawake wajisikie wanaweza
"Kutokana na uwezo uliopo ndani ya mwanamke basi leo tumeamua kuwa tunaweza kumjengea Mungu madhabahu kupitia kongamano hili" alisema
Amesema katika kanisa hilo wato watoto zaidi ya elfu moja ambao wanafundishwa maadili kupitia neno la Mungu kuibua vipawa mbalimbali vilivyopo ndani yao na kuviibua.
Toa Maoni Yako:
0 comments: