Mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga Iringa Damas Mgimwa akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi wakati wa kukata utepe wa kufngua choo hicho.
Mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakikagua ubora wa vyumba vya vyoo hivyo.
Hili ndio jengo jipya la choo kipya kilichojengwa na Tosamaganga Alumni Association kwa gharama ya shilingi millioni 30.
Hawa ni baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo.

Na Fredy Mgunda.

Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo kwa kuwa ndio umekuwa msingi bora wa mafanikio ya wanafunzi wengi waliosoma katika shule hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi choo hiyo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa lengo ni kukikisha kila wakati wanatafuta pesa za kusaidia kukarabati shule hiyo kutokana na miundombinu ya sasa si rafiki kwa wanafunzi.

Mbilinyi aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa aliwataka wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya hiyo wawe vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali kurudisha fadhila katika shule hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: