IMG_6547
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Usukani Bw.Martin Gabone akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Ziara yao ya kuwatembelea wagonjwa pamoja na kutoa misaada mbalimbali katika kitengo cha Moi-Muhimbili jijini Dar es salaam
IMG_6544
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Usukani Bw.Martin Gabone wa kwanza kushoto akiwa na wanafunzi wake ambao wanasomea mambo ya udereva walipofanya Ziara yao ya kuwatembelea wagonjwa pamoja na kutoa misaada mbalimbali katika kitengo cha Moi-Muhimbili
IMG_6554
Mwanafunzi kutoka Taasisi ya Mwanamke Usukani, Mary Kihanga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) akielezea namna walivyoweza kujitolea kwa ajili ya kusaidia wagonjwa mbalimbali katika hospitali ya Muhimbili.
IMG_6571
Mwakilishi wa Polisi WP Saburi Chutto wa kwanza kushoto wakimsikiliza mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya Muhimbili
IMG_6573
Wanafunzi toka Taasisi ya Mwanamke Usukani wakisubiri kutoa damu kwa ajili ya wagojnwa mbalimbali katika Kitengo cha Moi
---
Taasisi ya tiba na mifupa Muhimbili MOI imewashukuru taasisi ya Wanawake Usukani kwa kwenda kutoa misaada mbalimbali katika kitengo hicho ambacho ni muhimu kwa jamii.

Afisa uhusiano wa taasisi hiyo Patrick Jonh amesema hayo leo jijini Dar es salaam alipotembelewa na taasisi hiyo kwenda kuchangia damu kwa wagonjwa wanaohitaji damu, kwani katika kitengo hichi kina uhitaji mkubwa wa damu ili waweze kusaidia wagonjwa.


Kupitia mkurugenzi wa kampuni ya Wanawake Usukani Martin Gabone ambae anendesha mradi wa kuwajengea wanawake uwezo amesema kuwa wamenda kutoa misaada hiyo kwani kupita taasisi hiyo wanawake wanafursa ya kujifunza udereva hivyo ni chachu hata wao pindi watakapopata ajali waweze kusaidiwa kama leo walivyofanya wao pia iwe kioo kwa watu wengine waweze kwenda kuchangia damu na kutoa misaada.


Aidha aliongeza kuwa jamii inabidi iondokane na dhana ya kwamba wanawake hawawezi kuamua jambo, kwani sasa kuna fursa nyingi ambazo wan awake wanaweza kujikomboa kiuchumi na hata kijamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: