Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby.
Madaktari pamoja na Waganga nchini wametakiwa kutumia weledi wa taaluma yao katika kuhudumia wagonjwa hususani wafanyakazi wanaoumia kazini kwa kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa madaktari na waganga kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi nchini WCF na kufanyika katika ukumbi wa BOT Jijini Mwanza.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Madaktari pamoja na Waganga ili kutambua namna bora ya kufanya tathimini kwa mfanyakazi aliyeumia akiwa kazini.
Dkt.Abisalam Omary ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za tiba na tathimini WCF, amesema mfuko huo unawajengea uwezo madaktari hao ili kufanya tathmini sahihi kwa wagonjwa wanaoumia kazini ama wasaidizi wao.
Rehema Kabongo ni Meneja wa Mafao ya Fidia Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi (WCF) anasema kuwa "Tangu mpango huo ulipoanza mwaka 2015 kila uchwao maajiri wamekuwa wakifumbuka macho na kuona haja ya kujiunga na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kiasi kwamba wengi kwa makundi wameanza kujiunga na mfuko"
"Bado tunapata changamoto katika kutoa elimu kwa sababu mfuko huu bado ni mpya lakini tumejipanga kuhakikisha tunawafikia mmoja mmoja au kwa makundi ili kufikia malengo tuliyojiwekea yenye tija kwa matabibu wetu"
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba WCF, Dr. Abdullssalaam Omary akitoa maelezo kwa ufupi jinsi mfuko huo ulivyonuia kuleta mabadiliko kwa watumishi sekta ya afya.
“Tunataka hawa madaktari wawe na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kufanikisha azma yetu, na tumeamua kuwa mafunzo ya aina hii yatakuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kuwapatia muongozo utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kufanya tathmini,” alisema.
Mbali na madaktari na watumishi walio katika sekta ya afya wengi wa wafanyakazi waliopatwa na matatizo hayo kazini wanatoka sekta mbali mbali kama migodi, viwanda na usafirishaji.
Mfuko huo umeingia mkataba na watoa huduma za afya kwenye hospitali na vituo vya afya zaidi ya 6,000 nchi nzima ambapo zitahudumia wafanyakazi hao.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi akifunga mafunzo hayo hii leo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Christopher Juma kutoka Hospitali ya Nyamagana baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Christina Nyandwi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Frighton Rwechungura kutoka Hospitali ya Nyakahanga baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya huduma za tiba Dr. Boniphace P. Mayala kutoka Hospitali ya Rulenge baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Hongera mdau wa afya baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Hongera mdau wa afya baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: