Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabulla akiongea na wakazi wa kijiji cha Singa wilaya ya Mkalama mkoani Singida na kuwahakikishia kumaliza mgogoro wa mpaka uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 kati ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida na wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Wakazi wa kijiji cha Singa wilaya ya Mkalama mkoani Singida wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabulla wakati akiwahakikishia kumaliza mgogoro wa mpaka uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 kati ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida na wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Wakazi wa kijiji cha Singa wilaya ya Mkalama mkoani Singida wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabulla wakati akiwahakikishia kumaliza mgogoro wa mpaka uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 kati ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida na wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabulla ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Singida ambapo ametembelea wilaya ya Mkalama na kukutana na wananchi ambao walimfikishia kero zao za migogoro ya ardhi.
Wananchi hao walitoa kero zao mbele ya Naibu Waziri huyo ambapo wamemueleza mgogoro huo ambao ni wa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 30 na umeleta maafa makubwa kwa wakazi wa wilaya ya Mkalama Mkoani Singida uliopakana na wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Mheshimiwa Mabulla amemuagiza Kamishna wa Ardhi wa Kanda ya kati kushirikiana na ofisi ya wilaya ya Mkalama kutatua mgogoro huo kwa kupitia kigingi kwa kigingi cha mpaka huo.
Aidha Mheshimiwa Mabulla amewataka wananchi kuacha kuuza maeneo yao kiholela na badala yake wayapime maeneo yao na kupatiwa hati za kumili ardhi, kwa kuwa ardhi ni mtaji wa kudumu na unaopanda thamani kila siku.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla anaendelea na ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Singida, Manyara na Morogoro yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi kwa kukagua mabaraza ya ardhi, kukagua mfumo wa malipo ya kodi na kukutana na watumishi wa idara za ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: