Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) akiwa sambamba na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi
wanawake mkoani Iringa (TPF)
Kamanda wa Jeshi lapolisi mkoa wa Iringa, Julias Mjengi na mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF)
Hawa ni baadhi ya wanamtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) wakiwa katika maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa kwa mwaka 2007.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa lengo la kufanya kazi kwa ukaribu na jamii.

Akisoma risala iliyoandaliwa na mtandao huo, PC Doroth Matinde alisema kuwa mtandao wa polisi wanawake Tanzania (TPF) ulianzishwa mnamo tarehe 25 / 10 / 2007 kwa lengo la kuendelea kuifanya kazi kwa karibu kwa jamii na kufanikisha azma ya utekelezaji wa majukumu yake.

“Lakini ukiangalia na yote hayo lengo na malengo mengine ni kuunganisha askari wa kike kuwa karibu na jamii ili kudumisha mahusiano mema kati ya mtandao na wananchi hatimaye kuboresha huduma bora na kufanikisha ufanyaji kazi wetu” alisema Mtinde

Mtinde alisema kuwa mtandao huo wa polisi wanawake umekuwa ukitembelea akina mama wajane, kuwafariji na kuwapa msaada wa chakula ndani ya kambi za polisi hapa mkoani Iringa.

Aidha Mtinde alizitaja kazi watakazozifanya kazi katika cha maanzimisho watafanya usafi katika maeneo ya soko kuu manispaa ya Iringa,stendi kuu pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi mbalimbali wa shule za msingi na sekondari ili kuzuia uhalifu na kutoa elimu ya madhara ya madawa ya kulevya na mimba za mashuleni.

Kwa upande wake mgeni rasmi Ritta Kabati aliupongeza mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa kufikisha miaka kumi ya kuwatumikia wananchi na kuhakikisha wazitatua changamoto zilizowakabili wananchi na kuifanya jamii kuendelea kuishi kwa Amani.

Kabati aliwachangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kufanikisha shughli za mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) na kuhaikisha anawatafutia wafadhi wa kusaidia kutatua changamoto ili kuifikia jamii kwa urahisi Zaidi.

“Mimi natoa hiki kidogo tu lakini nitahakikisha nawatafuta wafadhili wengine ili kuendelea kuuchangia mfuko wa huu mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa ajili kuweza kuifikia jamii na kufanikiwa kutatua changamoto kwa haraka Zaidi” alisema Kabati.

Kabati aliliomba jeshi la polisi mkoani Iringa kuhakikisha wanapeleka dawati la jinsia katika shule za msingi na sekondari ili kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi kwa kuwa watakuwa wazi kuzungumza wanachofanyiwa huko mitaani.

Naye kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi alisema kuwa jeshi la polisi hapa nchini lipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mpango wa kulipeka dawati la jinsia kwenye shule za sekondari na shule za msingi kwa lengo la kuanza kutoa elimu mapema za ukatili wa kijisia.

“Ulicho kiongea mgeni rasmi ni kweli tatizo lipo sana mashuleni hivyo tuanza mikakati ya kuahikisha tunawafikia wanafunzi katika ngazi zote” alisema Mjengi

Mjengi alimpongeza mbunge Ritta kabati kwa juhudi zake za kulisaidia jeshi la polisi mkoani Iringa kwa hali na mali kwa kuwa amekuwa mstali wa mbele kutatua changamoto za jeshi hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: