Katibu wa chama akizindua jiwe la msingi la  ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Sinza "A"  Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM)  Salum  Kali akishiriki ujenzi wa ofisi za chama kata ya Sinza A.
 Katibu wa jumuia ya wazazi mkoa wa rukwa ndg chollaje nae alishiriki ujenzi huo.
 Katibu wa wilaya akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  kata ya sinza Shafii Diwani.
 Katibu wa wilaya akiwa kabidhi kadi wanachama wapya walio jiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kutoka vyama mbalimbali.
 Mmoja wa wazee wa Chama Cha  Mapinduzi  Wilaya ya Ubungo Bi siwema  akitoa nasaha kwa wanachama wenzake.
Viongozi wa jumuia ya umoja wa wanawake (UWT)  kata ya Sinza   wakishangilia.

Na Ripotawetu wa Globu ya Jamii

Katika kuazimisha kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo cha hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Chama Cha Mapinduzi(CCM) katibu wa chama wilaya ya ubungo , Salum kali ameweka jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za chama katika tawi la sinza "A"

Akiutubia wanachama walio jitokeza katika shughuli hiyO kali amesema, Baba wa taifa alitengeneza heshima kwa Mtanzania aheshimu kwanza maadili ya taifa lake ndio aweze kuheshimiwa na watu wengine.

aidha kali amesema kuwa , Mwalimu Nyerere aliamini ndani ya chama cha mapinduzi CCM ndiko kunapo patikana viongozi bora ambao wana uwezo wa kufanya kazi kwa umakini pasipo malumbano wala fujo kama tunavyo ona kwa wenzetu wa pembeni.

"Mwalimu Nyerere aliamini viongozi wa ccm pekee ndio wanao weza kusimamia amani ya nchi hii na ndio kitu ambacho mpaka sasa chama cha mapinduzi kinaendelea kufanya kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli" amesema Kali.

katibu kali amesema Baba wa Taifa alitengeneza upendo huku akidumisha amani kubwa ambapo mataifa mengi walikuwa wakimtumia Mwalimu Nyerere kwa kutafuta Amani katika nchi zao na wengi kuja kusoma na kujifunza Tanzania ili waweze kwenda kusaidia nchi zao, alitolea mfano moja ya nchi ya Msumbiji na nyingine nyingi ambazo zilikuja kujifunza nchini kwetu.

Aidha ameongeza kuwa sisi leo tunashindwa kukumbuka maadili na misingi ya Baba wa taifa aliyo iweka akiwa na nia ya kutuunganisha watanzania wawe kitu kimoja, pia waipende nchi yao , wapende maendeleo ya taifa lao ili tusonge mbele.

Pamoja na hayo katibu kali alizidi kusema Baba wa Taifa aliamini mno kwenye uaminifu, uadilifu na uwajibikaji huku akiwatilia mashaka wale wote walio kuwa wanataka kwenda ikulu kwani alichokua anaamini Baba wa Taifa kuwa URAIS ni utumwa ila alishangaa kuona watu wanagombania kwenda ikulu.

Adha katibu kali alisema walio zaliwa mwaka 1974 watakumbuka ilikuaje , lakini watu wanasahau sana , sasa ivi vijana wa Kitanzania wanabeza Taifa la TANZANIA linalo ongozwa na ccm, kwa kusema maisha magumu , huku vijana hao wakiwa wamekaa na kazi hawataki kufanya badala yake wamekuwa wakilala mika kwenye mitandao kuwa maisha magumu aliwaomba vijana na kuwasihi kufanya kazi kwani akuna kitu kinacho kuja bule na wasipende kudanganywa .

Alimalizia kwa kusema kwa mwendo wa wa mwenyekiti wake wa chama cha mapinduzi CCM ambae pia ni Rais wa Tanzania ana uhakika kabisa mpaka kufikia mwaka 2020 upinzani Tanzania utabaki kuwa ni mavumbi kwani haoni kazi zozote ambazo wabunge wa upinzani wakifanya zaidi ya vurugu na kwamba hata wakifanya bado wanatekeleza irani ya chama cha mapinduzi ccm alitoa rai kwa wana ccm wote kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi Baba wa taifa kwa vitendo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: