Vyama vya Fatah na Hamas vya Palestina jana Alhamisi vimesaini rasmi makubaliano ya upatanisho na ushirikiano, yaliyofikiwa mjini Cairo nchini Misri kupitia mkutano wao na waandishi wa habari.

Katika hali hii, Mkuu wa ujumbe wa Chama cha Fatah katika makubaliano hayo “Azzam al-Ahmad” amesema kuwa, yamefikiwa makubaliano kamili ya kuwezesha dhana ya kurudi kwa serikali ya Palestina na uhalali wake, katika kufanya kazi za kawaida na kusimamia Ukanda wa Gaza.

Aidha “Al Ahmad” katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na mkuu wa ujumbe wa Chama cha Hamas “Saleh Al-Arouri” ameongeza kusema kuwa, yamefikiwa makubaliano ya kuiwezesha serikali hilo, kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazotumika katika taasisi,wizara na jumuiya zote mjini Gaza bila kubagua, huku serikali ikisimamia kikamilifu vivuko vyote.
Ameweka wazi kwamba, wamekubaliana na idara ya vivuko ikiwa ni pamoja na upande wa Israel au ihusuyo kivuko cha Rafah,ambacho suala lake ni maalumu kwani kinahitaji taratibu fulani zinazohusisha uboreshaji wa majengo yake upande wa Misri,kwa kiwango ambacho kitaendana na hadhi ya Misri na pia taifa la Palestina ili kifanya kazi vizuri, huku mipango ya usalama ikisimamiwa na Mamlaka halali ya Palestina.

Vilevile ametangaza kuwa ulinzi wa Rais uttakuwepo pia upande wa mpaka wa Misri,huenda hatua hiyo isiwe kwa uharaka sana isipokuwa kwa vivuko vingine itakuwa ya haraka katika muda usiozidi Novemba Mosi ijayo, huku kila kitu kikipangiwa tarehe maalumu kwa ratiba.

Kwa upande wake, Rais wa Mamlaka ya Palestina “Mahmoud Abbas”, amepongeza mafanikio hayo yaliyopatikana katika mazungumzo kati ya Fatah na Hamas, yaliyofanyika mjini Cairo nchini Misri ambayo ndio iliyofadhili. Amesema hatua hiyo itaimarisha na kuharakisha hatua za kukomesha mgawanyiko na hatimae kurudisha umoja wa Wapalestina, ardhi na taasisi zake.

Aidha,Rais pia ameielekeza serikali yake,mashirika na taasisi zote, kufanyia kazi kwa bidii yale yote yaliyokubaliwa,huku akitoa wito kwa makundi na wadau mbalimbali kufanya juhudi katika kufikia kile kinacholengwa na Wapalestina ambacho ni kurejesha umoja wao. Rais amemshukuru Rais wa Misri “Abdel-Fattah Al-Sisiy”, kwa jukumu kubwa lililobebwa na nchi yake katika kufikia mafanikio haya muhimu.
Kwa upande mwingine, Rais Abbas amepokea pongezi kwa njia ya simu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa “Antonio Guterres”, kwa hatua hiyo nzuri inayolenga kumaliza mgawanyiko na hatimae kurudisha umoja wa kitaifa wa Palestina, iliyofikiwa mjini Cairo. Huku akisisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa katika kufanya kazi na Rais Abbas na Mamlaka yote ya Taifa ya Palestina, kuunga mkono jitihada za kuunganisha safu ya Wapalestina na kupunguza mateso ya watu wa Ukanda wa Gaza.

Kwa upande wake, Jumuiya ya Kiarabu imepongeza hatua hiyo iliyofikiwa na Palestina kati ya Hamas na Fatah chini ya ufadhili wa Misri, hatua ambayo itarudisha suala la Palestina katika mazingira ya kimataifa,huku Jumuiya hiyo ya Kiarabu pia ikiipongeza serikali ya Palestina inayoongozwa na Rais “Mahmuud Abbas” na wote waliohusika katika kufikia hatua hiyo nzuri, inayoimarisha msimamo wa Palestina dhidi ya changamoto zinazokabili suala la nchi hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa, makubaliano hayo yanahesabiwa kuwa ni dhamana ya msingi ya kufikia malengo ya taifa la Palestina, ikiwemo kupata uhuru wake kamili, kumaliza uvamizi wa Israel katika ardhi ya Palestina na hatimae kusimamisha dola huru yenye mji mkuu wake Jerusalem ya Mashariki, kwa mujibu wa mipaka ya Juni 4 mwaka 1967.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: